Header Ads Widget

HALMASHAURI YA ITIGI YAVIALIKA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA, WALEMAVU KUKOPA MIL.442.755/-

 


Thobias Mwanakatwe, ITIGI


HALMASHAURI ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida imetoa wito kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kuchangamkia kuomba mikopo ambapo zaidi ya Sh.ilioni 442.755 zimetengwa kwa ajili ya kutoa mikopo hiyo kwa vikundi hivyo.z


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi,Ayoub Kambi, akizungumza leo (Oktoba Mosi, 2024) na vijundi vya wajasiriamali, wazee wa kimila,wazee maarufu,watumishi na wananchi, amesema fedha hizo zilianza kutengwa katika robo ya kwanza ya Julai-Septemba ya mwaka wa fedha 2024/2025. 


"Halmashauri ya Wilya ya Itigi inatangaza uwepo wa fedha kwa ajili ya kuvikopesha vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ambapo jumla ya Sh. 442,755,221.17 zimetengwa, vikundi vyenye sifa vinakaribishwa kuleta maombi katika Ofisi za serikali za Vijiji zilizopo katika maeneo yao," amesema.


Kambi amesema vikundi vinavyotakiwa kuomba mikopo ni kile ambacho kinatambuliwa na kupewa cheti cha utambuzi na halmashauri, kinachojishughulisha na shughuli za ujasiriamali mdogo au wa kati au kikundi kinachotarajia kuanzisha shughuli za ujasiriamali.


Amesema sifa nyingine  kwa kikundi cha wanawake na vijana lazima kiwe na idadi ya wanakikundi kuanzia watano na kuendelea na kikundi cha watu wenye ulemavu kiwe na wanakikundi wasiopungua wawili . 


"Kwa kuzingatia kanuni ya 7 (1) mtu mwenye ulemavu anaweza kuwa na sifa ya kupata mkopo kama kikundi cha watu wenye ulemavu endapo timu ya menejimenti ya halmashauri itajiridhisha kuwa amekosa mtu mwingine mwenye ulemavu wa kuungana naye katika eneo lake," amesema.


 Mkurugenzi huyo amesema sifa zingine ni kikundi kiwe na akaunti ya benki iliyofunguliwa kwa jina la kikundi kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kiujasiriamali na wanakikundi lazima wawe ni raia wa Tanzania wasio na ajira rasmi, wenye akili timamu na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.


"Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kieletroniki (tembelea tovuti: mikopohalmashauri.tamisemi.go.tz) ili kutambuliwa na kuomba mkopo au wasiliana na Afisa Maendeleo ya Jamii wa kata husika au mtendaji wa kata husika," amesema Kambi.


Amesema kikundi kinachoomba mkopo kinapaswa kuwa na viambatisho ambavyo ni barua ya kikundi ya kuomba mkopo iliyopitishwa na Afisa Mtendaji wa kijiji, muhtasari wa kikundi wa kuomba mkopo, andiko rahisi la mradi unaoombewa mkopo kwa kuzingatia fomu iliyo ndani ya mfumo na taarifa ya akaunti ya benki.


Serikali ilisitisha mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kupitia Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,  Aprili 13, 2023 wakati akihitimisha hoja ya makadirio ya maombi na matumizi ya fedha kwa mwaka 2023/2024.


Ilipofika Aprili 6,Waziri Ofisi Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa,alitangaza kurejeshwa kwa mikopo hiyo wakati akisoma bajeti ya wizara yake mwaka 2024/2025.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI