Header Ads Widget

TCRA YAIFUNGIA MWANANCHI DIGITAL ..




Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) dhidi ya Mwananchi Communications Limited kwa kuchapisha maudhui yaliyokatazwa mtandaoni. 

TCRA, taasisi ya serikali inayosimamia huduma za mawasiliano, imesitisha kwa muda leseni za huduma za maudhui mtandaoni za kampuni hiyo kwa kipindi cha siku 30, kuanzia tarehe 2 Oktoba 2024.

Hatua hii imechukuliwa baada ya Mwananchi Communications Limited kuchapisha maudhui mjongeo na sauti yaliyokiuka Kanuni ya 16 ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2020, ambayo inakataza kuchapisha maudhui yanayolenga kudhihaki au kuharibu taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 TCRA imesema kuwa maudhui hayo yameleta tafsiri hasi kwa taifa, hali inayoweza kuathiri umoja, amani, na mshikamano wa kitaifa.

TCRA imetangaza kwamba wakati wa kusitisha leseni hizi, masuala mengine ya kiusimamizi yatashughulikiwa, na umma umejulishwa juu ya uamuzi huo.


HATA HIVYO KATIKA TAARIFA YAKE KWA UMMA MWANANCHI IMETANGAZA KUPOKEA AGIZO HILO NA KUSITISHA HUDUMA YA UCHAKATAJI MAUDHUI MTANDAONI 

Tunasikitika kuwaarifu wasomaji wetu wapendwa kuwa tunalazimika


kusitisha uchapishaji wa maudhui mtandaoni kuanzia sasa kufuatia

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kusitisha leseni zetu za utoajiwa huduma ya maudhui mtandaoni kwa siku 30 kutokana na kuchapisha maudhui yaliyozuiwa yanayokiuka Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni za Mwananchi Communications Limited (MCL) inaahidi kuwaletea wateja na wasomaji wetu habari, taarifa na maudhui bora yanayowezesha taifa kupitia magazeti yetu, na huduma zetu nyingine zisizo za mtandaoni wakati tukiendelea kuzungumza na mamlaka husika ili kupata muafaka. Tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa nasi.


Mpoki Thomson Mhariri Mkuu Mtendaji Msaidizi na Mhariri Mtendaji, The Citizen



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI