Na Elizabeth Ntambala Matukio Daima
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha takribani milioni 583.5 kwa ajili ya Mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Lanchi iliyopo katika Kijiji cha Mtowisa Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Hayo yamesemwa Oktoba 2, 2024.
na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt.Pindi Chana (Mb) mara baada ya uzinduzi wa shule hiyo.
"Ninafurahi kwamba fedha takribani bilioni 42 zimefika kwa wananchi na katika shule hii zaidi ya shilingi milioni 500 zimeletwa hapa" amesisitiza Mhe. Chana.
Amesema Serikali ya Rais Samia ni Serikali makini na imeelekeza fedha zifikishwe kwa wananchi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mhe. Chana amewaasa Wazazi kuhakikisha watoto wanapelekwa shule kwa kuwa Urithi wa Mtoto ni elimu.
Kwa Upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Lanchi, Augustin Mwambopo amesema mradi huo umesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na umeboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Pia amesema umesaidia wanafunzi wanaotoka mbali na eneo la shule na kupunguza matukio ya utoro shuleni.



.jpg)
.jpg)




0 Comments