NIOMBE Wote kuwa Makini na utapeli huu wa Promotion ya UNICEF tambua kuwa UNICEF- (United Nations Children’s Fund) ni shirika la Umoja wa Mataifa linalojikita katika kulinda haki za watoto na kuhakikisha wanapata mahitaji ya msingi kwa maendeleo bora.
Shirika hili linafanya kazi katika maeneo mbalimbali, yakiwemo:
1. Afya ya Watoto na Mama
Kupambana na magonjwa ya kuambukiza kama surua, polio, na malaria.
Kutoa chanjo na huduma za afya kwa watoto na wajawazito.
2. Elimu ya Watoto
Kuhamasisha elimu bora na fursa za kusoma kwa watoto wote, hususan wasichana na watoto wa mazingira magumu.
Kujenga na kusaidia shule pamoja na kutoa vifaa vya kufundishia.
3. Lishe Bora
Kupambana na utapiamlo kwa kutoa lishe ya dharura na elimu ya lishe bora kwa familia.
Kutoa msaada
Halihusiki na michezo ya bahati na sibu hivyo ni vema kuchukua TAHADHARI na utapeli Unaoendelea wa kutumia makundi ya Whatsapp kupitia namba za watu wenye ushawishi kuonesha wameshinda PROMOSHENI na kuhamasisha watu kujiunga .
MTATAPELIWA MCHANA KWEUPE OGOPA MATAPELI
By Matukio Daima media
0 Comments