Na Shemsa Mussa
Kagera .
Wananchi Mkoani Kagera pamoja na Viongozi mbali mbali wamesikika wakipiga Vigelegele na shangwe nyingi wakati wakimpokea Mkuu wa Mkoa wa huo Hajat Fatma Mwassa katika Uwanja wa ndege Bukoba akitokea Mkoani Mwanza akiwa amebeba kikombe na cheti maalum baada ya Mkoa wa Kagera kuibuka kinara Katika mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2024.
Baada ya kiongozi huyo kuwasili Katika viwanja hivyo alisikika akisema Kagera piga kelele itoshe kusema Kagera Baba lao huku shangwe zikisikika kila kona Mkoani humo.
Aidha aliongeza kuwa juhudi za ushindi huo zilitokana na wanaKagera kujitoa kwa nguvu zao zote maarifa yao yote na akili zao huku wakiikataa nafasi ya nyuma na kuitaka nafasi ya mbele ambapo wameipigania na kuipata.
Mkoa wa Kagera uliibuka kinara kwa kupata nafasi ya kwanza kwa kufanya vizuri katika kusimamia shughuli za maendeleo na shughuli za mbio za Mwenge wa uhuru.
Ushindi huo ulitangazwa kupitia kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2024 Mkoani Mwanza kilichoendana na hitimisho la wiki ya Vijana na kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere oktoba 14, 2024.
Aidha ujumbe Mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2024 ulijikita kwenye uhifadhi wa Mazingira na uhamasishaji wa uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Hata hivyo Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 zitazinduliwa rasmi Mkoani Pwani na kuzimwa Mkoani Mbeya ambapo ndio Mkoa utakaofanya shughuli za kilele cha mbio za Mwenge.
0 Comments