Header Ads Widget

SEKTA YA UTALII YAPATA MAFANIKIO, ONESHO LA SITE2024 LAHITIMISHWA DAR




Na Fatma Ally Matukio DaimaApp


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Pindi Chana amesema sekta ya utalii inachangia asilimia 17 ya pato la Taifa huku ikiingiza fedha za kigeni dola bill 3.6 sawa na asilimia 25.


Hayo ameyasema jijini Dar es Salaam Mapema leo hii wakati akifunga onesho la 8 la utalii wa kimataifa la kiswahili (Site 2024) ambalo limekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wanunizi wa kimataifa wa bidhaa za utalii.


Amesema kuwa, onesho hilo limepata wanunizi wa kimataifa wa bidhaa za utalii takribani 120, washiriki  mbalimbali kutoka nchi 50,pamoja na kampuni za kufanya maonesho  zipatazo 120.


"Utalii na ulinzi wa rasilimali zilizopo Tanzania ni vipaumbele kwa kila mtanzania lazima tuzitunze na tuzihifadhi kwani utalii unachangia pato la taifa katika kuleta maendeleo ya nchi"amesema Waziri Dkt Pindi.


Ameongeza kuwa, linapokuja suala la utalii watu wengi wananufaika  nalo wakiwemo watu wa mahoteli, madereva, wakulima wadogo wadogo, mashirika ya ndege ikiwemo ATCL ambapo huchangia mnyororo wa thamani kuwa na faida kubwa.


Aidha, amesema Tanzania kuna vivutio vingi ikiwemo mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi Afrika,utalii wa fukwe na malikale na hifadhi zisipongua 21 na makumbusho zisizopungua 7 ndani ya Taifa la Tanzania.


Sambamba na hayo amesema Tanzania ni kisiwa cha amani ambapo watalii wanaongezeka kutokana na amani iliyopo hali inayopelekea nchi hiyo kuwa mfano wa kuigwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii TTB Balozi Dr Ramadhani Dau amesema kwenye utalii Kuna mambo mawili kuhifadhi na kutangaza ambapo jukumu la Ttb ni kutangaza vivutio lakini kuhifadhi ni jukumu la kila moja wetu .


Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuhifadhi vivutuio vya utalii kwani watalii wanapokwenda nchini humo Kata za Halmashauri zao wanapata mapato, hivyo amewataka waendelee kutunza vivutio hivo.


"Jukumu la uhifadhi lipo kwa kila moja wetu Tanzania kwa sababu kama watu watahamia kwenye hifadhi watachoma moto watatuharibia miundombinu na matokeo yake watalii watapungua kuja nchini kwetu"amesema Balozi Dr Dau

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI