Na Matukio Daima media
MKUU wa mkoa wa Iringa, Peter Serukamba ataka mafunzo kwa madaktari kuhusu tathimini za Ulemavu kutokana na ajali na magonjwa ya kazi yatumike kuwajenge zaidi madaktari .
Mkuu huyo wa mkoa ametoa pongezi hizi leo mjini Iringa wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum kwa madaktari kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Songwe, Rukwa, Mbeya, Katavi, na Ruvuma, kuhusu tathmini za ulemavu unaotokana na ajali na magonjwa ya kazini.
Katika mafunzo haya ya Siku tano yanayoendelea katika ukumbi wa Royal Palm mjini Iringa kuanzia 28 Oktoba hadi 1 Novemba 2024 mkuu huyo wa mkoa alitaka washiriki kuzingatia Mafunzo hayo .Serukamba alipongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kuandaa mafunzo hayo muhimu.
Kuwa mafanikio ya sekta ya ajira nchini Tanzania yanategemea afya na ustawi wa wafanyakazi, hivyo kuimarisha uwezo wa madaktari kufanya tathmini ya ajali na magonjwa yanayotokana na kazi ni hatua muhimu katika kulinda nguvu kazi ya Taifa.
Mkuu wa mkoa alisema kuwa WCF ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoanzishwa Julai 2015 chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ikilenga kusimamia Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi (Sura 263).
" Jukumu kuu la mfuko huu ni kuhakikisha wafanyakazi waliopata ajali au kuathirika kiafya kutokana na mazingira ya kazi wanapata fidia stahiki"
Kuwa WCF inatoa mafao saba makuu, ikiwa ni pamoja na malipo ya huduma za matibabu, fidia ya ulemavu wa muda na wa kudumu, huduma za utengemao, malipo kwa wasaidizi wa wagonjwa, fidia kwa wategemezi wa mfanyakazi aliyefariki, na msaada wa mazishi kwa wafanyakazi waliopoteza maisha kutokana na kazi.
Alisema hadi sasa, WCF imetekeleza majukumu haya kwa ufanisi na kulipa mafao ipasavyo.
Akizungumzia umuhimu wa mafunzo haya, Serukamba alisema kuwa yanalenga kuwapa madaktari ujuzi wa kipekee ili kuhakikisha wanufaika wa fidia wanapata huduma bora za afya.
" Madaktari pia watafundishwa kufanya tathmini sahihi za ulemavu wa muda au wa kudumu unaosababishwa na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi, sambamba na utambuzi wa magonjwa yanayohusiana na kazi"
Alisema hadi sasa, madaktari 1,606 wamepata mafunzo ya awali, na wengine 133 wamepatiwa mafunzo ya vitendo.
Kuwa mafunzo haya yanasaidia madaktari kuboresha huduma na kuongeza ufanisi katika tathmini za ulemavu," alieleza Mkuu wa Mkoa.
Serukamba aliwakumbusha madaktari kuwa ushiriki wao katika mafunzo haya ni muhimu kwa ajili ya kuhuisha leseni zao za kitaaluma, kupitia alama za Maendeleo Endelevu ya Taaluma (CPD Points).
"Utendaji bora wa madaktari utakuwa msaada mkubwa kwa Mfuko wa Fidia na utasaidia wafanyakazi kurudi kazini mapema.
Kuwa hii itasaidia kuongeza tija na uzalishaji kwa Taifa," alisisitiza . Serukamba.
Mkuu huyu alisema kuwa mafunzo hayo yanafanyika kwa mzunguko katika kanda mbalimbali nchini, huku mafunzo ya sasa yakilenga mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na mikoa jirani.
Alisema kuwa Iringa inajivunia kuwa mwenyeji wa mafunzo haya muhimu kwa mara hii, akiongeza kuwa anatarajia madaktari waliopata mafunzo watatoa mchango mkubwa katika utoaji wa huduma bora kwa wafanyakazi.
Serukamba aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kufuatilia kwa makini mada zitakazowasilishwa na kutumia maarifa watakayopata kuboresha huduma kwa wafanyakazi walioumia au kuathirika kiafya kazini.
"Ni muhimu kuhakikisha kwamba wafanyakazi wanapata huduma stahiki na fidia kwa wakati. Mafanikio ya sekta ya ajira yanategemea ustawi wa afya ya wafanyakazi wetu," alihimiza.
Pia aliwaasa madaktari kuhakikisha wanatambua na kutibu magonjwa yanayotokana na kazi ipasavyo, huku wakizingatia miongozo na sheria zinazotawala fidia kwa wafanyakazi.
Awali akimkaribisha mkuu huyo wa mkoa mkurugenzi wa WCF Dr. John Mduma alisema kuwa mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (Workers Compensation Fund - WCF) ni taasisi ya hifadhi ya jamii chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Alisema kuwa Mmfuko huu ulianzishwa mnamo Julai 2015 kwa lengo la kutekeleza Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Sura ya 263.
"Jukumu kuu la WCF ni kulipa mafao kwa wafanyakazi wanaopata ajali au magonjwa kutokana na kazi wanazofanya, iwapo mfanyakazi anafariki kutokana na kazi, fidia hulipwa kwa wategemezi wa marehemu"
Kuwa WCF hutoa jumla ya mafao saba ambayo ni malipo ya huduma za matibabu,Malipo ya ulemavu wa muda, Malipo ya ulemavu wa kudumu na Malipo ya huduma za utengemao
Malipo mengine ni malipo kwa mtu anayemsaidia mgonjwa asiyeweza kujihudumia,Malipo kwa wategemezi wa mfanyakazi aliyefariki kutokana na kazi na Msaada wa mazishi kwa mfanyakazi anayefariki kutokana na kazi
Kuwa hadi sasa, WCF imekuwa ikitoa mafao haya kikamilifu kwa mujibu wa sheria.
Akielezea lengo la Mafunzo hayo alisema kuwa WCF imekuwa ikitoa mafunzo kwa madaktari kote nchini ili kuhakikisha wanufaika wanapata huduma bora za afya na tathmini sahihi za ulemavu.
Kuwa hadi sasa, madaktari 1,606 wamepata mafunzo ya awali, huku wengine 133 wakipata mafunzo ya vitendo juu ya tathmini ya ulemavu (impairment assessment).
USIKOSE KUTAZAMA HABARI YA KUTWA NZIMA KUPITIA CHANEL YA MATUKIO DAIMA TV LEO USIKU IWAPO UNAHITAJI KUTANGAZA NASI PIGA SIMU 0754026299
0 Comments