Header Ads Widget

RC MAKONDA AHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA

 


Na,Jusline Marco;Arusha

Wakazi wa Mkoa wa Arusha wamehimizwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la Mkazi ili kuweza kupata sifa za kushikiri kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba 27 ya mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ametoa wito huo baada ya kukagua zoezi la uandikishaji kwenye vituo mbalimbali Jijini Arusha,ambapo amewataka wananchi kufahamu kuwa maendeleo ya Taifa lolote yanaanzia ngazi ya Kitongoji na Kijiji.

Akiwa kwenye Kituo cha kujiandikishia wananchi kilichopo kwenye Ofisi ya Mtendaji Kata ya Moivo Jijini Arusha, Mhe. Makonda amewaambia wananchi wa eneo hilo na mkoa kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi huo ili kuwapata viongozi waadilifu na wenye kutanguliza mbele maslahi ya umma.

Uchaguzi wa serikali za Mitaa unatarajoa kufanyika Novemba 27, mwaka huu chini ya Kaulimbiu ya Serikali za mitaa,sauti ya wananchi,shiriki uchaguzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI