Cheti Cha pongezi ;Mwalimu Lulu Shayo Mkuu wa Shule ya Msingi Kiomboi Hospitali iliyopo katika Kata ya Old Kiomboi, Wilaya ya Iramba mkoani Singida akimkabidhi Mwanahabari Mathias Canal Cheti cha utambuzi wa shughuli za maendeleo katika shule hiyo
Na Matukio Daima media,Iramba
MKONO utoao ndio hupokeao hakika naamini katika usemi huu maana usijiulize kwa nini unafanikiwa katika mambo yako ukajua na kwa nguvu zako kumbe wapo wanaokesha wakikuombea kwa kuwa kidogo unachokipata unakigawa kwa wengi.
Ni waandishi wa habari wachache nchini Tanzania wenye moyo wa Kuchangia jamii kwa fedha kiasi wanayoipata kwenye kazi ya Kalamu yao wakiamini kuwa wao ni watu wa kupokea na kuandika Fulani Kuchangia hiki .
Si Dhambi kutochangia ila tambua huwezi kufanikiwa bila kuchangamana na jamii na sio vibaya kutoa sadaka kwa Kijiji chako ama shule uliyosoma kwa Kila kidogo unachokipata .
Mathias Canal si tajiri wa mali bali ni tajiri wa moyo wa kujitolea kwa kidogo alichonacho akiamini Uwekezaji kwenye Mioyo ya watu .
Canal ni mwandishi wa habari wa WazoHuru Media amekuwa mstari wa Mbele kuhamasisha jamii kwa kuchangia maendeleo katika shule aliyosoma Kijijini kwake kiomboi Wilaya ya Iramba.
Pamoja na kuendelea Kuchangia maendeleo ya shule hiyo Canal amewataka wananchi wa mkoa wa Singida kuendelea kumuunga mkono Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwa juhudi kubwa anazofanya kwa maendeleo ya Tanzania.
Canal anawataka wananchi waendelee kumuombea na kumpa ushirikiano ili Dkt. Mwigulu afanikishe malengo yake ya kuboresha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Oktoba 2, 2024, katika mahafali ya 73 ya Shule ya Msingi Kiomboi Hospitali, iliyopo kata ya Old Kiomboi, wilayani Iramba, Singida anasema kuwa Kazi ya Dkt. Mwigulu inayopaswa Kuungwa Mkonoa alieleza kuwa kazi za Mbunge huyo ni nzito, na kutokuwepo mara kwa mara jimboni haimaanishi uzembe, bali ni ushahidi wa juhudi zake katika kushughulikia majukumu makubwa kitaifa.
“Sisi wanyiramba tuna bahati kuwa na Mbunge ambaye ni Waziri wa Fedha.
Dkt. Mwigulu ni mchumi mbobezi aliyehudumu kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na nafasi mbalimbali serikalini kama Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Kilimo, Mambo ya Ndani, na Katiba na Sheria.
Pia ni mjumbe wa NEC na amehudumu kwenye Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM). Hivyo, tunapaswa kumtia moyo kwa kazi kubwa anayofanya," alisema Mathias.
Mathias pia alitoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta ya elimu nchini.
Aliipongeza jitihada za kuanzisha mafunzo ya miezi mitatu kwa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba kabla ya kujiunga na kidato cha kwanza, akisema utaratibu huu utachochea mshikamano na kuimarisha uelewa wa wanafunzi.
Michango kwa Shule ya Msingi Kiomboi Hospitali katika kuunga mkono maendeleo ya elimu, Mathias Canal alichangia jumla ya shilingi milioni 4.26. Michango hiyo ilihusisha madawati 36 yenye thamani ya TZS 3,060,000
Vifaa vya michezo kama Jozi nne za jezi na mipira minne, jumla TZS 800,000
Huku Diwani wa Old Kiomboi Sadick Msengi, alichangia madawati matano, kuonyesha mshikamano wa uongozi wa kijamii na juhudi za kuimarisha elimu.
Zulfa Alli ni mmoja wa wazazi wa wahitimu shuleni hapo anapongeza jitihada za Mathias Canal katika Kuchangia maendeleo ya shule hiyo na kutaka viongozi na wadau wengine waliopo nje ya wilaya hiyo kurudi kuwekeza nyumbani kwa kidogo wanachopata .
Husein Alli ambae ni mkazi wa wilaya ya Iramba anasema kijana huyo kaonesha mfano kwa wengine na sio kwamba anapesa Kuliko wengine ila anatumia pesa yake kidogo kujibana kula na wengine .
0 Comments