Header Ads Widget

RC DENDEGO AKIPONGEZA KIWANDA CHA BIOSUSTAIN TANZANIA LTD KWA KUSAIDIA MIRADI YA MAENDELEO

 


Na Thobias Mwanakatwe,SINGIDA 


MKUU wa Mkoa wa Singida,Halima Dendego,amekipongeza kiwanda cha pamba kinachomilikiwa na Kampuni ya Biosustain Tanzania Limited kwa jinsi ambavyo kimekuwa karibu na serikali na kuisaidia jamii kwenye miradi ya maendeleo.


Alitoa pongezi hizo juzi baada ya kufanya ziara ya kukitembelea kiwanda hicho kuangalia jinsi kinavyofanya kazi.


"Niwashukru sana menejimenti ya Biosustain Tanzania Limited kwasababu mumekuqa karibu sana na serikali ya mkoa, wilaya na Manispaa ya Singida,mnaisaidia sana jamii mimi ni shuhuda nilikwenda Mtekente kwenye sekondari iliyopo pembezo nikakuta mumejenga bweni na vyoo," alisema.


Dendego akizungumzia uzalishaji wa pamba, alisema serikali ya Mkoa wa Singida itahakikisha inaweka mikakati ya kuhamasisha wakulima kuweka mkazo katika kilimo cha pamba mkoani hapa ili kiwango cha uzalishaji kiweze kuongezeka na kufikia zaidi ya kilo milioni sita.


Alisema hayo baada ya kuelezwa kuwa kiwango cha uzalishaji wa Pamba katika Mkoa wa Singida kimeshuka kutoka kilo milioni sita hadi kufika kilo milioni 2.5 mwaka.


"Hatukubali kuona uzalishaji wa pamba unashuka kwa kiwango hiki,lazima tukaweke mpango mkakati wa wakulima wetu ili uzalishaji uweze kuongezeka na kufikia zaidi ya kilo milioni 6,"alisema Dendego na kuipongeza kampuni ya Biosustain Tanzania Limited kwa uwekezaji mkubwa iliofanya katika kiwanda hicho.


Mkuu wa Mkoa alisema serikali itatoa ushirikiano wa karibu katika mpango unaofanywa na kampuni hiyo wa kutaka kujenga kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kula yanayotokana na mbegu za pamba.


Dendego alisema Mkoa wa Singida unategemewa sana katika suala la uzalishaji wa mafuta ya kula ya alizeti hivyo kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kula yanayotokana na mbegu za pamba litakuwa jambo zuri sana na kufikia ndoto ya serikali.


"Sisi Singida tumejipambanua kuhakikisha hili goli la dhahabu ambalo tumepewa kuweka vikwazo kwa mafuta ya kula kutoka nje ya nchi kuingia nchini kwa kuongeza tozo hii bi fursa kwetu ya kuhakikisha tunazalisha mafuta kwa wingi",alisema.


Aidha,Mkuu wa Mkoa aliipongeza kampuni ya Biosustain Tanzania Limited kwa kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi ambao ni wanawake na kamba utaratibu huo unaakisi agenda ya kufikia asilimia 50 kwa 50.


Naye Mratibu wa Shughuli za Kilimo wa kampuni ya Biosustain Tanzania Limited,Bether Bryton, alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa mafanikio yaliyopatika katika kipindi cha 2024 ni kuwa na wafanyakazi wa kudumu 139  na  vibarua 310 na hivyo kuwa na wafanyakazi wapatao 410. 


Katika shughuli za kilimo Kampuni imeweza kuajili wagani (extension Officers) wapatao 56 na pia inahudumia wagani 48 wa kutoka mradi wa Jenga Kesho iliyo bora (Building Better Tomorrow) kwa Pamoja kupata huduma zote kama wagani ikiwa na mishahara, vyombo vya usafiri (pikipiki) na mafuta ili kurahisisha kufanya shughuli za kilimo. 


Bryton alisema mpaka sasa kampuni ina jumla ya wakulima 24,000 ambao wanauwezo wa kuzalisha pamba mbegu (seed cotton) kilo milipni 44 ambayo inaweza kuleta pamba nyuzi kilo milioni 18 kwa mwaka.


 Alisema changamoto iliyopo katika kilimo ni baadhi ya wakulima kuongeza mchanga,mawe na maji katika pamba haii inayosababisha kuharibu ubora wa mbegu na pamba lakini pia hupelekea kutokidhi viwango na ubora wa pamba unaohitajika katika masoko ya ndani na nje ya nchi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI