Jina la P-Diddy au Diddy Limekuwa Midomoni mwa Watanzania Wengi Hivi Sasa Kutokana na Tuhuma Zinazomkabili Nguli Huyo wa Muziki Nchini Marekani, Hata Hivyo Taarifa Zinazohusiana na Tuhuma Zake Zimekuwa za Kuchanganya.
Inaelezwa Kuwa Neno P-Diddy au Diddy Linatafutwa Zaidi Kwenye Mitandao ya Kijamii Tanzania Kuliko Ilivyokuwa Likitafutwa Hapo Awali Kabla ya Tuhuma Zake, Pia Mauzo ya Nyimbo Zake Yamekuwa kwa Zaidi ya Asilimia 18 Duniani.
Kabla ya Kuelewa Kuhusu Tuhuma Zinazomkabili Bwana Diddy Hebu Tumfahamu kwa Ufupi, Japo Amekuwa Akibadili Majina Yake Lakini Huitwa Sean Combs na Majina Yake Mengine Maarufu ni P-Diddy, Diddy au Puff Daddy.
Mzaliwa Huyo wa Mwaka November 4, 1969 Jijini New York Alisoma Kuhusu Masuala ya Biashara Katika Chuo Kikuu cha Howard Kabla ya Kuanza Harakati za Kujitafuta Katika Muziki kwa Kutumia Hasira ya Maisha ya Familia Yake.
Bwana Combs Kwenye Kazi Zake za Muziki Alikuwa Pia Meneja wa Wasanii Mbalimbali na Kisha Mwaka 1993 Akafungua Lebo Yake ya Muziki Bad Boy Entertainment Iliyochangia Mafanikio Makubwa Katika Usimamizi wa Wasanii.
Mwaka 1997 Mwamba Huyu Aliachia Albamu Yake ya Kwanza ‘No Way Out’ Iliyopata Mafanikio Makubwa na Kushinda Tuzo Nyingi Ikiwamo Tuzo Maarufu Duniani za Grammy, Diddy Amehusika Kwenye Nyimbo Nyingi Kubwa Duniani.
Diddy ni Maarufu kwa Sherehe Zake Zinazoitwa ‘White Party’ Zinazofanyika Kila Mwaka na Kuhudhuriwa na Watu Mashuhuri Ulimwenguni, Sherehe Hizi Ambazo Wahudhuriaji Wake Huvaa Mavazi Meupe Ndio Kiini cha Tuhuma Zinazomkabili.
Lakini Pia Msela ni Mfanyabiashara Mwenye Mafanikio Makubwa Marekani, Anamiliki Kampuni ya Mavazi ya Sean John, Kampuni Nyingine Anazomiliki Zinahusika na Vileo, Hifadhi ya Hoteli, Teknoloji Pamoja na Masoko ya Kidigitali.
Nguvu Yake Kwenye Sekta ya Burudani Marekani ni Kubwa Kutokana na Lebo Yake, Kuhusika Kwenye Utayarishaji wa Nyimbo Kama Mzalishaji, Kushiriki Kwenye Tasnia ya Filamu, Televisheni, Matamasha na Mashindano ya Vipaji.
Sasa Tuziangazia Tuhuma Ambazo kwa Namna Moja Au Nyingine Zimemfanya Kutawala Mijadala Sio Tu Tanzania Bali Pia Duniani Kote Kutokana na Habari Zake Kuchapishwa Kwenye Vyombo Vingi vya Habari na Mitandao ya Kijamii.
Sean ‘Diddy’ Combs Anakabiliwa na Tuhuma Tatu Nzito Hadi Sasa Japo Kuwa Kuna Uwezekano wa Tuhuma Hizo Kuongezeka Kutokana na Uchunguzi Unaoendelea Dhidi Yake, Watu Wengine au Taasisi Yoyote Aliyoshirikiana Nayo.
Tuhuma Hizo ni Uendeshaji wa Kundi la Uhalifu, Usafirishaji wa Wanawake Kwaajili ya Biashara ya Ngono na Unyanyasaji wa Kimwili kwa Kuhusika Kwenye Matukio Ambayo Hayana Kiswahili Fasaha Lakini Yakiitwa Freak Offs.
Matukio Hayo ni Kuwa Wanawake Ambao Wanajiuza au Wamekubaliana Kufanya Ngono Hulazimishwa Kufanya Ngono Zaidi ya Muda wa Kawaida au Makubaliano kwa Kushawishiwa Kutumia Dawa za Kulevya au kwa Kutishiwa.
Zaidi ya Wahanga 120 Wamejitokeza Kumshtaki Diddy kwa Kuwanyanyasa, Wakiwamo Wanawake, Wanaume na Watoto wa Chini ya Miaka 18 na Kwamba Tuhuma Hizo Zinahusisha Matukio Yaliyotokea Tangu Mwaka 1999 Hadi Sasa.
Tuhuma Hizo Zilizofunguliwa Katika Mahakama ya Kiraia Huko Manhttan Jijini New York Zilisababisha Bwana Combs Kukamatwa na Kuwekwa Mahabusu Katika Gereza Lenye Ulinzi Mkali Huko Brooklyn na Dhamana Yake Kuzuiwa.
Wakaguzi Baada ya Kufanya Upekuzi Kwenye Nyumba za Diddy Walipata Baadhi ya Vitu Ikiwamo Lita 1000 za Mafuta Ambayo ni Kirainishi, Walipata Silaha Mbalimbali na Risasi Sambamba na Kukamata Baadhi ya Dawa za Kulevya.
Ushahidi Huo Unaweza Kumwongezea Diddy Mashtaka Sababu Kesi Yake Awali Haikuhusisha Jinani na Ndio Sababu Ilifunguliwa Katika Mahakama ya Kiraia na Sasa Uchunguzi Ukibaini Ana Jinai Atafunguliwa Pia Kesi Mahakama za Kijinai.
Stori Kubwa Hapa Bongo Imekuwa Kiasi Kikubwa cha Mafuta (Virainishi) Yaliyokutwa Kwenye Upekuzi Nyumbani Kwake, Ina Aminika Mafuta Hayo Yamekuwa Yakitumika Kama Virainishi Wakati wa Matukio ya Hizo Freak Offs.
Kesi ya Diddy Inatarajiwa Kuanza Rasmi October 9, 2024 Lakini Jamaa Amekataa Mashtaka Yote na Anatumia Wakili Wake, Erica Wolff, Kujitetea na Anaendelea Kushikiliwa Mahabusu Huko Brooklyn Baada ya Mahakama Kuzuia Dhamana.
Ikiwa Tuhuma Zake Hazitajumuisha Makosa ya Jinai na Kuendelea Kushtakiwa Katika Mahakama ya Kiraia Basi Jamaa Adhabu Yake Kubwa Kama Atapatikana na Hatia Itakuwa Kulipa Fidia Tu ya Fedha kwa Waathirika na Sio Kifungo Jela.
Sasa Sababu Mamlaka Zinasema Zinaendelea na Uchunguzi Kubaini Ikiwa Matukio Hayo Yana Makosa ya Jinai, Basi Mwamba Atashtakiwa Kwenye Mahakama ya Jinai na Akikutwa na Hatia Adhabu ni Kifungu Kikubwa Gerezani.
Hizo Ndizo Taarifa Kuhusu Tuhuma za Mwamba Diddy, Bado Ana Muda wa Kujitetea Kuwa Hana Hatia Katika Mahakama Lakini Mawakili wa Walalamikaji Wamesema Watapambana Hadi Mwisho Ili Kutetea Haki za Walionyanyaswa.
Kuna Dhana Kwamba Diddy Anaonewa na Tuhuma Zake ni za Kupandikizwa Kutokana na Kwamba Yeye ni Mtu Mweusi Tajiri Nchini Marekani, Dhana Nyingine ni Kuwa Alijihisi ni Mtu Asiyeweza Kuguswa na Mkono wa Sheria.
Dhana Nyingine Inatajwa Kuwa Msimamo Yake Imeanza Kwenda Tofauti na Mifumo (So Called Matrix) Mfumo Unaoongoza Dunia kw Kila Jambo Hivyo Amepakaziwa Tuhuma Ili Kumshusha na Kudhibiti (Cancelation Stratagies).
Kuhitimisha Naweza Kusema Kuwa Wadosi Wamemnasa Kwenye Mtego Hatari na Kuchomoka Katika Mtego Huo Hata Ikiwa Mahakama Zitasema Hana Hatina Bado Kutakuwa na Athari na Tuhuma Zake Zitamtafuna Maisha Yake Yote.
Edwin Dugange.
Iringa-Tanzania
0 Comments