Header Ads Widget

RC ANDENGENYE ATOA MAELEKEZO KUHUSU MPOX KIGOMA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma



MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amesema kuwa mkoa Kigoma ni moja ya mikoa iliyo kwenye hatari ya watu wake kupata maambukizi ya ugonjwa wa nyani maarufu kama MPOX hivyo ametoa ilani kila mmoja kuchukua tahadhari.

 

Andengenye alisema hayo kwa viongozi wa dini na vyama vya siasa ambao alikuwa akifanya nao mkutano kuhusu masuala ya uchaguzi na kubainisha kuwa ni vizuri kila mmoja kuchukua tahadhari sasa kabla ugonjwa huo hauajaingia mkoa humo.

 

Alisema kuwa mkoa Kigoma unapakana na nchi ya Kidemokrasi ya Congo upande wa mashariki ya nchi hiyo ambayo ndiyo sehemu kubwa yenye muingiliano na Tanzania na hivyo mkoa Kigoma kama lango la kuingia na kutoka katika eneo hilo inapaswa kuchukua tahadhari kubwa kwa watu wake ili ugonjwa huo usiingie mkoani Kigoma na kuleta madhara.

 

“Kwa sasa hakuna Mgonjwa ambaye amesharipotiwa lakini serikali na idara ya afya inachukua hatua mbalimbali za kudhibiti kuingia kwa ugonjwa huo ikiwemo kutoa elimu ya hatua za kuchukua ikiwemo kunawa mikono kila wakati, kutoshikana mikono na kutowaficha ndani wagonjwa wenye dalili hiyo,”alisema Mkuu huyo wa mkoa.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI