Header Ads Widget

DC KUBECHA AMEWAHASA WANANCHI KUJITOKEZA KUSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI

Na Ashrack Miraji (Matukio Daima App)

Akizungumza leo  na waandishi wa habari ofisini kwake, Mhe. Kubecha alisema, "Ni muhimu kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuchagua viongozi watakaokuwa chachu ya maendeleo katika wilaya na Mkoa wetu wa Tanga."

Hivyo nitumie fulsa hii Kuwasihi Wananchi wa Tanga Tujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Aidha, aliwakumbusha waandishi wa habari kuendelea kutoa taarifa kwa umma, akisisitiza umuhimu wa kuandaa vipindi vya kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu faida za uchaguzi wa Serikali za Mitaa. "Tunapaswa kuchagua viongozi wenye uelewa na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya," aliongeza.

"Viongozi wa Serikali wametakiwa kufanya kazi kwa pamoja katika kuhamasisha wananchi kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa, huku wakitaja kauli mbiu ya uchaguzi huu: "Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi. Jitokeze Kushiriki Uchaguzi."A

Alisema kubecha Mkuu wa Wilaya ya Tanga

.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI