Header Ads Widget

RAIS DKT SAMIA NI KIONGOZI KIELELEZO KWA VIONGOZI WANAWAKE NCHINI

WANAWAKE viongozi nchini wametakiwa kujifunza kuongoza kutoka kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ni kielelezo cha Uongozi imara, hodari, makini, madhubuti na uliotukuka nchini katika utendaji kazi katika sekta na nyanja Kiongozi mwanamke anaongoza.


Hayo yamesemwa wakati wa kufunga mafunzo ya Uongozi  na usimamizi Jumuishi na endelevu kwa wanawake 30 waliyoyapata katika shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kwamfipa Kibaha mkoani Pwani akimwakilisha Wahitimu wa mafunzo hayo Naomi Zegezege.

Amesema kozi mbalimbali na Mafunzo yanayotolewa Shuleni hapo ya kuwajengea uwezo wa Uongozi kundi la Wanawake Viongozi ni kwa agizo la Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hivyo alimshukuru kwa uanzishwaji wa mafunzo hayo na kuhakikisha Wanawake Viongozi wanapata elimu hiyo iliyokusudiwa.


Walisema kupitia mafunzo hayo Wanawake Viongozi wamejifunza kujitofautisha mtu na taasisi, kuboresha mahusiano kazini, viongozi na Serikali pamoja na kuwa na Taasisi zenye kufanya kazi kwa ufanisi na bila kusahau kutimiza wajibu wao katika familia zao wao wakiwa ni Viongozi na Mama wa familia.

Alisema wataenda kuwa na ujasiri wa kufanya kazi zao na kuondoa dhana ya kwamba mwanamke ni mpaka awezeshwe.


Aidha amesema mafunzo hayo yanahitajika mara kwa mara kwa kundi la Wanawake Viongozi kwani ni moja ya sehemu ya kuwajenga kuwaimarisha katika uongozi wao na kuwa vinara wa utendaji katika taasisi wanazoongoza.

"Mafunzo haya ni sehemu ya Maagizo ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan ambayo amekuwa akihimiza Wanawake wapate mafunzo mbalimbali ya kujimarisha katika kazi zao na sisi tunaahidi kwenda kuleta mabadiliko kwenye nafasi zetu," alisema Zegezege.


Akitoa neno la shukrani za dhati wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samis Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi anazofanya kuhakikisha wanawake wanajengewa uwezo ili waweze kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia serikalini, katika mashirika ya umma, sekta binafsi na hata katika shughuli mbalimbali za kujipatia kipato ilikuendeleza uchumi wa nchi yetu.

Aliuhsema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazothamini mchango wa mwanamke katika uongozi na ngazi mbalimbali za kiutendaji na hivyo Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa maelekezo katika majukwaa mbalimbali yanayohusu mwanamke kuwa ni lazima wanawake wajengewe uwezo kupitia mafunzo mbalimbali yanatolewa na vyombo vyetu vya elimu au majukwaa mbalimbali ili waweze kugombea nafasi mbalimbali na pia kupewa majukumu makubwa ya kuongoza pale inapobidi. 


"Washiriki tumejifunza masuala muhimu ya Uongozi kwa upana kuanzia maeneo muhimu yanayowezesha shughuli za serikali kufanyika bila kuingiliwa kama vile masuala ya Usalama wa Taifa tukianzia na ulinzi wa mipaka, na raia wake, umuhimu wa upatikanaji wa huduma za jamii, pia  historia ya ukombozi wa Afrika ili tujue nchi imetoka wapi, iko wapi na inaelekea wapi," alisema Naomi.

Zegezege alisema "ili kutumia fursa hii ni lazima wanawake tutambue kwamba tuna mwanamke wa kwanza aliyejitoa kugombea nafasi ya uongozi kwa kujiamini na amefanya kazi kwa bidii na uadilifu wa hali ya juu na kuonesha uwezo wake mkubwa na hatimaye kuaminiwa na mamlaka za juu serikalini na kufanyika kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Mwanamke na na hatimaye kuwa Rais wa kwanza Mwanamke wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla".


Aidha Mwenyekiti huyo alihoji kwakusema tusipojifunza kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa kwanza Mwanamke Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla tutajifunza kutoka wapi tena? 

Afisa Mkuu rasilimali watu kutoka benki ya NMB Emmanuel Akonay  alisema mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kutatua vikwazo vinavyowakabili na kuleta matokeo chanya sehemu zao za kazi.


Mkuu wa shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Profesa  Marcellina Chijoriga  alizishukuru Taasisi zilizowaruhusu wafanyakazi wao Wanawake kushiriki mafunzo hayo huku akiwataka kuwa mabalozi Wazuri kuhusiana na masomo yanayotoleiwa shuleni hapo.

Wanawake hao pia walikumbushwa kuzingatia uchapakazi, uadilifu katika kazi zao  na pia kuwa wajasiri kwenye maeneo yao, uzalendo na ubunifu kwa manufaa ya Taasisi zao na nchi kwa ujumla.


Mambo mengine waliyojifunza ni kutambua kwamba wanawake wanaweza kuchangia nini katika uongozi katika jamii na mambo mengine ya kujenga timu yenye nguvu ya umoja na utekelezaji wa maagizo ya serikali, Masuala ya utawala bora, Masuala ya kuandaa mipango kazi, ukusanyaji wa fedha na utafutaji wa mapato; namna ya kujenga sura nzuri ya serikali kwa ujumla kupitia Taasisi wanazozitumikia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI