Header Ads Widget

ACT WAZALENDO WABAINISHA SABABU ZA ZANZIBAR KURUDI NYUMA KIMAENDELEO

Na. MWANDISHI WETU

Mwenyekiti wa Chama cha Act Wazalendo Taifa Othman Masoud alisema Zanzibar imerudi nyuma kimaendeleo tangu kukwamishwa mpango wa Zanzibar kuanza kusajili kampuni za kimataifa na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.


Othman Masoud alisema hayo  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Ditia Wawi Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.


Alisema mwaka 1996 Serikali iliajiri kampuni moja toka nchini Uingereza waje kusaidia kutengeneza mfumo wa usajili wa kampuni za kimataifa ili Zanzibar iweze kufanya kazi hiyo kwa malengo ya kuimarisha uchumi wake.


“Walikuja wakaandaa na mswada wa sheria na taratibu zote  mimi wakanichukua wakanipelekea uingereza kwa takrabani miezi miwili wakinifundisha kusimamia jambo lile lakini wenzetu wakalikwamisha,”


Akifafanua Zaidi alisema baada ya jambo hilo kufikishwa katika kamati ya baraza la wawakilishi baadhi ya wajumbe walitaka kujua kama Serikali ya jamhuri ya muungano imesharuhusu jambo hili kufanyika aliekuwa waziri wa fedha Balozi Amina Salum Ali alijibu “ndio tumeruhisiwa”


Hata hivyo balozi Amina katika kuwaridhisha wajumbe Zaidi aliamua kufunga safari Tanzania bara kuonana na aliekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Prof Kigoma malima ili ampe barua rasmi ya kuruhusiwa lakini aliandikiwa barua kwamba Zanzibar haiwezi kufanya jambo hili kinyume na kauli za awali.


Alisema kwamba, Zanzibar haiwezi kupiga hatua mbele za maendeleo kama vyanzo vya Msingi vya maendeleo vikiendelea kubakia kuwa orodha ya mambo ya muungano kama vile kodi ya ushuru wa forodha, ushuru wa bidhaa, mafuta na gesi na usafiri Bahari Kuu.


Nae Makamu Mwenyeiti wa Chama cha Act Wazalendo Ismail Jussa Ladu amesema bajeti kuu ya Serikali kutegemea kodi ya huduma kila mwaka inachangia kuzorotesha sekta ya biashara Zanzibar na kuongeza ugumu wa maisha kwa Wananchi wake.


Alisema Zanzibar hivi sasa kuna nuka njaa Wananchi wanashindwa kumudu milo mitatu kutokana na kuporomoka kwa sekta ya biashara jambo ambalo limesababisha kupungua kwa mzunguko wa fedha.


“Bajeti ya Zanzibar chini ya Serikali ya CCM zimekuwa bajeti za kugawana umasikini na kuwanufaisha wakubwa na matumbo yao ambayo hayajai wala hayashibi, bajeti ya nchi ili na maana lazima ipandishe viwango vya Maisha ya wanayoishi watu lakini ipunguze gharama za Maisha ya watu hiyo ndio bajeti,”


Alisema kila mwaka ikisomwa bajeti Wananchi wakishuhudia kuongezwa kwa kodi na kumuongezea ugumu wa Maisha mwananchi kutokana na serikali kutegemea kodi ya huduma badala ya uzalishaji.


Alisema kwamba, kuna nchi za visiwa kama Zanzibar zimeanza kujenga uchumi mzuri huku pato la wananchi wake kwa mwaka likiendelea kuongezeka na mwananchi kuishi Maisha ambayo yanapaswa kuishi binadamu.


“Leo chukuwa kisiwa cha shelisheli  kidogo sana pato lake la mwananchi kwa mwaka ni dola 12,200, Mauritius  pato lake dola elfu 10, Singapore dola elfu 67 wakati Zanzibar wastani wa kodi ya mwananchi dola elfu 12 kwa mwaka sawa na Dola 100 kwa mwezi,”


Alisema Zanzibar kuna vitendio vya ufisadi wa kutisha kwa mujibu wa ripoti za mdhibiti na mkaguzi  Mkuu wa hesabu Serikali (CAG) na kutoa mfano ufisadi uliofanyika katika ukarabati wa uwanja wa gombani kisiwani Pemba.


Alisema CAG alibaini kuwa gharama za ukarabati huo zilikuwa ni shilingi Bilion 2.8 lakini ghafla gharama zikapandishwa na kufikia shilingi Bilion 5.64 sawa na ongezeko la asilimia 1000.


Mwenyekiti wa Chama cha Act Wazalendo Othman Masoud ameendelea na mikutano ya hadhara na kutumia muda mwingi kukosoa msimgi ya demokrasia na utawala bora licha ya kuwa makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar katika Serikali ya umoja wa kitaifa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI