Header Ads Widget

NACHINGWEA KUFANYA BONANZA LA KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA

 


Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea amesema wanatarajia kufanya bonanza la kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki kikamilifu uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji 27/11/2024.


Akizungumza na mwandishi wetu,kaimu mkurugenzi Joshua Mnyang'ali alisema kuwa bonanza hilo linalenga kutoa elimu ya kushiriki kikamilifu uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji katika wilaya ya Nachingwea.


Mnyang'ali alisema kuwa bonanza hilo litafanya siku ya jumamosi 5/10/2024 katika uwanja wa majengo ambao michezo mingi itafanyika huku kukiwa na  wasanii mbalimbali wakipamba jukwaa la burudani kwa wakazi wa wilaya ya Nachingwea.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI