![]() |
| Niccolò Machiavelli, mwanafalsafa wa karne ya 16, anafahamika kwa maoni yake kuhusu siasa na uongozi, yaliyoelezwa kwa kina katika kitabu chake maarufu, The Prince (Mfalme). |
Katika kazi yake hii, Machiavelli anashikilia kuwa Pamoja na mambo mengine anayetafuta madaraka lengo lake ni kuyashika madaraka na kuyadhibiti, bila kujali mbinu zinazotumiwa. Kwa mujibu wa falsafa yake, mbinu zozote zinazowezekana zinapaswa kutumika, iwe ni hila, nguvu, au fujo ili kuhakikisha kuwa anaingia madarakani.
Machiavelli anaamini kuwa siasa siyo suala la maadili ya kibinadamu, bali ni mchezo wa nguvu na ushawishi. (Nadhani ni kutokana na hili tukapata msemo maarufu “siasa ni mchezo mchafu”.
Aliona kuwa dunia imejaa vurugu na hila, na kwa hivyo, ili kiongozi au chama chochote kiweze kushinda na kuongoza, kinapaswa kutanguliza hila,ghilba na vurugu badala ya maadili.
Hii inajumuisha kutumia mbinu zisizo za moja kwa moja kama vile hadaa, kulazimisha ushawishi kwa kijamii, na wakati mwingine kutumia nguvu na vurugu.
Kimsingi, “lengo huhalalisha njia” ama kwa kiingereza, the end justifies the means ndiyo kauli maarufu inayohusishwa na Machiavelli.
Katika muktadha wa siasa za Tanzania, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetumia falsafa ya Machiavelli kutafuta madaraka ya nchi, huku viongozi wake wakitumia njia hizohizo kubakia madarakani ndani ya chama hicho.
HADEMA kimekuwa kikipigania kuingia madarakani kupitia njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na siasa za uhamasishaji wa harakati za kudai mabadiliko ya kidemokrasia.
Kujenga Mwamko wa Watu: Machiavelli anasisitiza umuhimu wa kuwa na uungwaji mkono wa umma.
CHADEMA imekuwa ikitumia mikakati ya kujenga uelewa na mwamko miongoni mwa wananchi kuhusu umuhimu wa mabadiliko.
Kufanya mikutano ya hadhara, midahalo, na kampeni za kidigitali ikiwa mbinu ya kuongeza umaarufu wa chama na kuhamasisha wapiga kura kuelekea mabadiliko.
Kutumia watu wenye ushawishi ambao husambaza uongo bila kushtukiwa kirahisi na wananchi.
Kujifanya Kusimama Kidete kwa Masuala ya Kijamii:
Katika mazingira ya kisiasa ya Machiavelli,ni muhimu kwa chama kutetea maslahi ya wananchi ili kupata uungwaji mkono.
CHADEMA imerukia masuala muhimu kama vile kupinga ufisadi, kudai haki za binadamu, na kudai kuimarishwa huduma za kijamii kama afya na elimu.
Kuwasilisha ajenda hizi kwa umakini na uhodari hadharani ili kuwafanya wananchi wawe na imani kuwa ni chama cha mabadiliko ya kweli.
CHADEMA kimejifanya kupinga ufisadi hadharani wakati chenyewe kimejaa ufisadi ndani yake na mara nyingi kikiishi kwa kunufaika n ufisadi wa nje yake.
Kujenga Ushawishi wa Kimataifa:
Machiavelli aliona umuhimu wa kujenga mahusiano ya kimataifa kwa ajili ya kushika utawala.
CHADEMA imetafuta uungwaji mkono wa kimataifa kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu, nchi zinazohimiza demokrasia, na asasi zisizo za kiserikali.
Wamefanya hivyo hata kwa kusema uongo, kujifanya wanakimbia nchi ili ionekane wanaonewa nyumbani na wameunga mkono mambo ya hovyo kama ushoga ili kuungwa mkono na mataifa yanyosukuma ushetani huo.
Ushawishi huu umesaidia chama kupata msaada wa kimkakati na kimtaji kwa kampeni zake.
Kutumia Mbinu za Hila Katika Kujipenyeza Serikalini:
Machiavelli alishauri kutumia hila, na wakati mwingine kufanya mapatano ya muda na maadui ili kujipenyeza na kuimarisha nafasi.
CHADEMA inaweza kutumia mbinu hii kwa kufanya maelewano ya muda na baadhi ya viongozi wa CCM wenye mtazamo tofauti, ili kuibua migogoro ndani ya chama tawala.
Inaweza kupewa taarifa za ndani ya serikali na baadhi ya maofisa wa serikali wenye manung’uniko nao wakazitumia kwa faida yao kujijenga ama kuikashfu serikali.
Kupitia mbinu ya mapatano ama maridhiano, wanaweza kupandikiza “makamanda”
wao wanaoteuliwa na kupewa nafasi ndani ya CCM na baadaye kuteuliwa serikalini na hili kutoa nafasi kwa CHADEMA kujipenyeza zaidi katika vyombo vya dola.
Kuunganisha Vyama Vingine vya Upinzani: Machiavelli anaeleza kuwa anayekusudia kushinda anapaswa kujenga umoja. Ili kufanikiwa kuingia madarakani, CHADEMA hutumia mbinu ya kuunganisha vyama vingine vya upinzani kama vile ACT-Wazalendo au NCCR-Mageuzi.
Kanuni inayotumika hapa ni ile ya adui wa rafiki yangu naye ni adui yangu. Umoja huu huwa ni wa hila na kwa hiyo huwa haudumu.
Kudhoofisha Sifa ya CCM Kupitia Uvumi: Machiavelli alipendekeza kutumia habari za uwongo au uvumi ili kudhoofisha hadhi ya wapinzani.
CHADEMA imekuwa ikitumia mbinu za ushawishi kupitia mitandao ya kijamii au vyombo vya habari binafsi ili kueneza habari za uvumi na uongo zinazodhoofisha uhalali wa CCM, iwe ni za kweli au za kupotosha.
Akaunti kama ile ya Gavana Balali, Kigogo, TanzaLeaks, Tanzagiza, ni mfano wa njama hii chafu.
Kushawishi Wafuasi wa CCM kwa Ahadi za hewa: Katika baadhi ya mifano ya kimachiavelli, chama cha upinzani kinaweza kuwahadaa wafuasi wa chama tawala kwa kuahidi manufaa makubwa zaidi, hata kama ahadi hizo hazitekelezeki.
Mfano CHADEMA ndiyo walianza kuhubiri habari ya elimu bure mpaka chuo kikuu, mikopo ya elimu ya juu kwa kila anayehitaji, Matibabu bure kwa wote na kadhalika.
Mbinu hii inaweza kuwavutia wapiga kura wanaotaka mabadiliko ya haraka au kutoridhishwa na chama tawala.
Kuvuruga Utulivu wa CCM Kupitia Machafuko: Machiavelli anashauri kuwa wakati mwingine ni lazima kuvuruga amani ili kufanikisha malengo.
CHADEMA imetumia maandamano au migomo ili kulazimisha serikali ya CCM kufanya makosa au kushughulikia mambo kwa njia inayowachosha wananchi, hali ambayo itafanya upinzani uonekane kama chaguo bora.
Wakati mwingine CHADEMA hutenda jinai kwa watu wake wenyewe ili kujenga huruma ama kuhamishia lawama kwa serikali (False Flag), au kufanya fujo makusudi ili viongozi wao wakamatwe na kufunguliwa mashtaka wapate sababu ya kushtaki nje ya nchi.
Ama kuifanya dola muda wote kukimbizana nao ili kudhoofisha uwezo wa serikali kuhudumia wananchi.
Mbinu za Kihila Katika Kampeni: Machiavelli anashikilia kuwa siasa ni mchezo wa hila na upinzani lazima uwe na uwezo wa kucheza mchezo huo.
CHADEMA imekuwa ikitumia mbinu za kisasa za kijasusi au mbinu za teknolojia kufuatilia harakati za viongozi wa CCM na kutengeneza mikakati ya kuwatia katika migogoro ya kisiasa au kuwapunguzia umaarufu mbele ya jamii.
Taarifa Potofu (Disinformation) Machiavelli aliamini kuwa ukweli unapaswa kuchujwa au kubadilishwa ili kuwavutia watu kwa manufaa ya kushika madaraka. Katika siasa za Tanzania:
CHADEMA imekuwa ikitumia mbinu za kueneza habari ambazo zinapotosha na za uongo kuhusu uwezo au uadilifu wa viongozi wa CCM, mfano, kueneza uvumi kwamba viongozi wa CCM wanahusika na ufisadi au wanachukua maamuzi yanayowakandamiza wananchi.
Zaidi wanaweza hata kumsingizia rais kuwa ni muuaji ili kuharibu sifa yake na chama kwa wananchi.
Kuvuta Vyombo vya Habari (Co-opting Media) : Udhibiti wa vyombo vya habari ni kipengele muhimu katika falsafa ya Machiavelli kwani vyombo hivi vina uwezo mkubwa wa kuunda maoni ya umma.
CHADEMA, kwa kuwa ni chama cha upinzani, inaweza kuvuta hasa Vyombo vya habari binafsi, hasa mitandao ya kijamii na vyombo vinavyoelekea kuwa huru, vinaweza kuvutiwa na mbinu za kidijitali au kuwapatia habari ambazo zinavutia hadhira, Mitandao ya kijamii imekuwa uwanja muhimu kwa upinzani kueneza habari mbadala, kuikosoa serikali, na kuwafikia wapiga kura wa kizazi kipya kwa njia za kisasa.
Aidha CHADEMA inaanzisha magazeti kwa kutumia watu binafsi kama ilivyo MwanaHalisi, MAWIO, ama kushawishi wahariri wa vyombo vikubwa, ama kudhibiti mitandao kama JamiiForum kwa Tanzania ambapo hujidai kutoa uhuru wa kuongea. Imegundulika kuwa uhuru unaoruhusiwa ni ule wa kuitukana serikali.
Makala yoyote yenye kuisema CHADEMA inafutwa. Hata makala hii inaweza kufutwa.
CHADEMA na Mitandao ya Kijamii: CHADEMA imeweza kutumia vyema mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, na YouTube katika kuwasilisha ajenda zake na kile wanachoita kufichua masuala ya kiufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu ndani ya serikali.
Kadhalika kila mara wanapiga makelele kuwaambia wafuasi wao kugomea vyombo visivyowaunga mkono kama TBC, Katika umachiavelli CHADEMA Kinatumia mazingira yasiyodhibitiwa sana na serikali kupotosha ili kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wapiga kura, hasa vijana.
Matokeo ya Mbinu hizi:
Machiaveli anashikilia kuwa matokeo ndio jambo la msingi. Mbinu yoyote inayohakikisha chama kinadhibiti mitazamo ya umma na kudhibiti taarifa zinazotolewa kwa wananchi inaweza kuwa na faida kubwa, hata kama ni ya hila au kupotosha.
CHADEMA tangu ianzishwe imetumia mbinu hizi za Kimachiaveli.
Kwa nini haijafanikiwa sasa pamoja na kutumia mbinu hizo kabambe?......... Wote tutafute jibu la swali hili.
Imeandikwa na Joseph Ludovick






0 Comments