Na Esther Machangu,Moshi Kilimanjaro
Wito umetolewa kwa wananchi kuwa na utaratibu wa kufuatilia matumizi Yao ya maji pamoja na kulipa Ankara za maji kwa wakati
Hayo yamebainishwa na watumiaji wa maji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Muwsa) leo oktoba 11,2024 Tumaini Masue na Laurance Chakusaga walipombelewa na watoa huduma wa mamlaka hiyo katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja.
Watumiaji hao wa maji wamebainisha kuwa endapo kila mtu atafuatilia kwa umakini malipo ya Ankara zake na kulipa kwa wakati hakutakuwa na malalamiko yoyote kwa mamlaka hiyo, pamoja na kuvilinda vyanzo vya maji ili huduma hiyo iwe endelevu.
Kwa upande wake meneja wa huduma kwa wateja kutoka mamlaka hiyo Mwanandani Mtonye, akimuwakilisha mkurugenzi wa huduma kwa wateja amesema katika maadhimisho ya siku hii ya huduma kwa mteja wamewatembelea wateja wanalipa Ankara zao kwa wakati bila usumbufu wowote pamoja na kutoa zawadi mbalimbali ili kuhamasisha wateja wengine kulipa kwa wakati
Aidha mtonyi amesema kuwa katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja mamlaka imetoa msamaha kwa wateja wote waliokatiwa maji watakapomaliza deni la maji katika maadhimisho haya watarudishiwa huduma ya maji bila kulipia gharama ya urejeshwaji wa huduma hiyo.
0 Comments