Header Ads Widget

CHADEMA NYASA WAHIMIZA KUJIANDIKISHA, WATUHUMU UKIUKAJI KANUNI.

 


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kanda ya Nyasa, kimewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la mkazi la wapiga kura ili kupata fursa ya kuchagua viongozi bora kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa baadaye mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CHADEMA kanda ya Nyasa Bi. Grace Richard Shio wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kadege jijini Mbeya.

Akizungumzia hamasa ya zoezi la uandikishaji, kiongozi huyo mtendaji wa CHADEMA kanda ya Nyasa, amesema ni wakati wa kila mwananchi kutumia siku kumi hadi Oktoba 20 kujiandikisha na kuchagua viongozi bora kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa akisema ndio msingi wa maendeleo unakojengwa.

"Ukiangalia msingi wote uko huko chini (Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji), viongozi tunaowapata wanahusika na masuala kuanzia masuala ya taka, hata masuala ya ndoa zikileta changamoto tunawaeendea wao (wenyeviti), masuala ya tozo mbalimbali mambo yote yananzia kule chini kwahiyo wanabeba sana madaraka pamoja na shughuli za kila siku za mwananchi katika maeneo husika hivyo ni muhimu kila mmoja wetu akajiandikishe kuanzia leo (Tar.11,2024 hadi tarehe 20 Oktoba, 2024 kila siku kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni", ameeleza Bi. Grace.

Amewahimiza pia wananchi mbalimbali wenye sifa na uwezo wa kuongoza kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye vijiji, vitongoji na mitaa mbalimbali kupitia Chama hicho ili watu kupata viongozi imara akisema CHADEMA imejipanga na ina uhakika wa zaidi ya asilimia themanini kushinda uchaguzi huo.

Pamoja na hayo kiongozi huyo ameeleza kutoridhishwa na mwenendo wa zoezi hilo katika siku ya kwanza ya uandikishaji wapiga kura kwenye daftari la mkazi ambapo amesema watendaji wameripotiwa kusimamia zoezi hilo tofauti na kanuni za uchaguzi jambo ambalo CHADEMA imekemea ikiwemo katika majimbo ya Mbarali, Kalambo na Kilolo mkoani Iringa.

"Zoezi la uandikishaji limeanza lakini kuna vitu kadhaa ambavyo haturidhiki navyo, moja ni watendaji wa mitaa, vijiji na kata kusimamia hili zoezi la uandikishaji. 

Kanuni ya 10:3 ya uchaguzi inasema watendaji mitaa na kata hawatateuliwa wala hawataruhusiwa kuandikisha au kuandaa orodha ya wapiga kura lakini katika vituo mbalimbali vya uandikishaji kuna watendaji wa vijiji, mitaa na kata ndio wanaosimamia hili daftari kinyume kabisa na kanuni hizi za uchaguzi wa Serikali za mitaa kwahiyo tunafikiri ifike mahali vyombo husika visimamie kile ambacho wamekitunga wamekipitisha kisimamiwe na hii ni changamoto ambayo tumeanza kuona kwenye suala la kuapisha mawakala na hata hivi kwenye vituo bado watu hawa wanaonekana kusimamia hilo zoezi", ameeleza Grace Shio, katibu wa kanda ya Nyasa (CHADEMA).

Sanjari na hayo, amewataka wanachama wa Chama hicho kuendelea kushikamana ili kuiishi falsafa yao ya CHADEMA ni nguvu ya umma kwa kuhakikisha wanaendelea kufanya kazi na kukitumikia Chama hicho na kukiletea

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI