Na Hamida Ramadhan, Matukio Dodoma App Dodoma
MKURUGENZI wa Shirika la Msichana initiative Rebecca Gyumi amesema licha ya jitihada zinazofanywa na shirika hilo kuweka usawa kwa mtoto wa kike, juhudi hizo hazionekani kuzaa matunda kwani Changamoto bado zipo hasa za kimitazamo, mila ,tamaduni na desturi kwa jamii nyingi ambazo zina mitanzamo hasi kwa watoto hao.
Hayo ameyasema leo jijini hapa Katika tamasha la Msichana Amani muziki festival lililowakutanisha shule 16 katika Kata ya lamaiti Wilayani bahi Dodoma ambapo ameeleza kuwa Shirika hilo(Msichana Initiative )kwa kushirikiana na mashirikia mengine sita wameamua kumfuata Msichana katika jamii na kuwafikishia ujumbe Moja kwa moja.
"Mfano mzuri katika Jamii tunazotoka utakuta mzazi anamshawishi mtoto wa kike afanye vibaya katika masomo yake ya mwisho ili akafanye kazi za ndani mjini na mshara anauchukua mzazi, wazazi wa aina hii huwa hawajiulizi future ya watoto wao itakuwaje," amesema.
Mkurugenzi huyo amezitaja Changamoto nyingine kuwa ni za kimfumo ikiwemo Sera na sheria ikiwemo sheria ya ndoa wamekuwa wakiipigia kelele na sarikali imekua ikichukua muda kuirekebisha na tunaona namna ambavyo inahamasisha ndoa za utotoni kwenye jamii.
" Tunaamini kupitia sherehe hizi za mtoto wa kike tutaendelea kuungana kama wadau kuhakikisha watoto wa kike wanapata haki yao stahki na ndio maana tunafika kule ambako watoto wapo hatubaki mjini tunafika kule watoto wapo na kunashida za mimba za utotoni, ndio za utotoni, na mumko mdogo wa elimu, " Amesema.
Ameeleza mpaka sasa wameshafikia watoto katika mikoa 10 nchini Tanzania na wasichana zaidi ya 5000 wamefikiwa tangu kuanza kwa harakati hizo.
"Tumeeona matuna na matokeo yameonekana japo Sio kwa kiasi kile tunachotamani kuiona hasa kwenye masuala ya uelewa kupitia haki zao, kuhusiana na fursa zilizopo katika jamii na nafasi zao kuweza kuonyesha uongozi na kuishi katika ndoto zao, " Amesema.
Mbali na hayo mkurugenzi huyo amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanakuza vipawa vya watoto hasa mtoto wa kike na kuwajenga kuwa viongozi .
" Nasema hivyo kwaana takwimu za HakiElimu kwenye masuala ya elimu zinaonyesha asilimia 85 ya vijana hawajawahi kushiriki katika maamuzi ya shule asilimia 68 ya wanafunzi hawajawahi kigombea nafasi mbalimbali za uongozi na asilimia 44 hawashiriki katika uchaguzi wa wanafunzi tuna haja kubwa ya kuwafanya watoto kupenda uongozi tangu watoto na kuona uongozi ni sehemu ya maisha yao"
Kwa upande wake Isaya Matata Afisa Tarafa wa Mdemu akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya bahi Rebecca Nsemwa Amesema Tamasha hilo ni muhimu na linakwenda kumuandaa mtoto wa kike kuwa kiongozi tangu utotoni.
Amesema ni wakati sasa wa watoto kike kugombea nafasi za uongozi mashuleni ili aweze kujiandaa kuwa kiongozi mkubwa wa baadae.
" Ili watoto wetu hasa wasichana washiriki katika fursa uongozi ni lazima jamii, wazazi na walezi kuwapeleka watoto shuleni kupata elimu na ndio mwanzo wa kujitambua na tuhakikishe wanafikia ndoto zao bila kusahau kuanza kushirikishwa kwenye maamuzi ya kifamilia, " Amesema Afisa huyo.
0 Comments