Header Ads Widget

WANAFUNZI ZAIDI YA 1000 SHULE YA MSINGI TUMAINI WAPATIWA HUDUMA YA VIPIMO NA ELIMU YA MAGONJWA YA MACHO BURE.

 



Matukio Daima App- Bukoba 


Wataalam wa Macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba wameendelea kuadhimisha Wiki ya Uoni Dunia  kwa kutoa huduma ya vipimo na elimu ya magonjwa ya macho bure  kwa Wanafunzi  zaidi ya 1000 wa shule ya msingi Tumaini iliyopo Manispaa ya  Bukoba mkoani Kagera.


Akitoa elimu ya magonjwa ya macho Egdius Karatunga alisema kuwa mwanafunzi yoyote  hawezi kufanya vizuri darasani kama haoni vizuri.


" Tunaamua kuadhimisha wiki ya uoni Dunia kwa kutembelea na kutoa huduma ya vipimo na elimu ya macho kwenye  baadhi ya shule zenye watoto wenye mahitaji maalumu,  mwanafunzi asipo ona vizuri hawezi kufanya vizuri darasani ndiyo maana tumekuja hapa ili muweze kujua hali ya afya ya macho yenu"


Aidha, amesema kuwa kupitia uchunguzi walioufanya baadhi ya wanafunzi wameonekana kuwa na tatizo la uoni hivyo wanahitaji dawa na wengine miwani huku akiwasihi wanafunzi hao kuacha michezo hatarishi inayoweza kuatarisha macho yao kama vile kurushiana mchanga machoni, kurushiana mawe na mifagio.



Kwa upande wake mwalimu mkuu wa Shule ya Tumaini Alfred Baganda amewashukuru wataalam wa macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Bukoba kwa kuichagua shule hiyo kuwa miongoni mwa shule zilizopata huduma ya macho bure huku akiahidi kuwa wanafunzi waliobainika kuwa na matatizo ya uoni atawasiliana na wazazi wao ili waweze kuwafikisha hospitalini kwa huduma zaidi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI