Header Ads Widget

KADA WA CHADEMA ALIYEANDIKA MTANDAONI KASHAMBULIWA NA WATU WASIOJULIKANA KUMBE ALIKUWA KALEWA

 

NA MATUKIO DAIMA APP 

Baada ya kujisambazia taarifa kwenye ukurasa wake wa X kuwa ameshambuliwa na kupigwa na watu Wasiojulikana aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Vijana chadema (BAVICHA) Kanda ya Nyasa Vitus Nkuna amekamatwa na polisi .

 Imeelezwa kuwa Nkuna alikuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa na kusababisha ajali na kushambuliwa na wenye gari aliloligonga .


Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa SACZP Alan Bukumbi akitoa aarifa kuhusu kukamatwa kwa kada wa Chadema mkoa wa Iringa Vitus Nkuna kwa kosa la kutoa taarifa za upotoshaji mtandaoni ya kuwa amevamiwa na kushambuliwa na watu wasiojulikana.

,SACP  Bukumbi amesema  kada huyo wa Chadema Vitus Nkuna mnamo Tarehe 30 Septemba 2024 katika eneo la Mgongo kata ya Nduli Barabara ya Iringa-Dodoma akiwa anaendesha gari aina ya Volkswagen Touareg yenye rangi nyeusi na mamba za usajili  T 797 DYC alisababisha ajali kwa kuligonga gari aina ya TOYOTA Probox yenye namba za usajili T 975 EDC mali ya kampuni ya KINGS.



Aidha baada ya ajali hiyo mtuhumiwa Vitus Nkuna alipimwa kipimo cha ulevi na kukutwa ana kiwango kikubwa cha kilevi katika damu yake kiwango ambacho hakikubaliki.



HAYA HAPA NI MADHARA YA  UNYWAJI POMBE KIPITA KIASI .

Madhara ya pombe kupita kiasi ni makubwa kwa afya na maisha ya mtu. Kwanza, husababisha matatizo ya ini kama vile ugonjwa wa ini kuvimba (cirrhosis). 


Vilevile, inaweza kuathiri ubongo, kupunguza uwezo wa kufikiri, na kuleta matatizo ya kumbukumbu. Pombe kupita kiasi pia huongeza hatari ya magonjwa ya moyo, saratani, na magonjwa ya tumbo.


 Aidha, inaongeza hatari ya ajali kutokana na kupoteza umakini. Kwa upande wa kijamii, pombe hupunguza tija kazini na kusababisha migogoro ya kifamilia pamoja na kuongeza uwezekano wa utegemezi (ulevi sugu).


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI