Header Ads Widget

POLISI YAKAMATA BUNDUKI YA KIVITA KIGOMA

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

POLISI mkoani Kigoma imekamata bunduki moja ya kivita aina ya AKA 47 ikiwa na risasi moja ikiwa imetelekezwa na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Mkesha wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.

 

Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Filemon Makungu akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari ya msako wa mwezi mmoja uliofanywa na polisi mkoani Kigoma alisema kuwa bunduki hiyo imesalimishwa ikiwa zoezi la kusalimisha silaha kwa hiari.

 

Kamanda Makungu alisema kuwa zoezi hilo ambalo limeanza Septemba Mosi mwaka huu linatarajia kukamilika Oktoba 31 mwaka huu ambapo alitoa wito watu wote wanaomiliki silaha isivyo halali kuzisalimisha na kwamba hakuna hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yao.


Akieleza dhumuni ya muda huo wa msamaha alisema kuwa unatokana na mkoa Kigoma kuwa na silaha nyingi zilizoingizwa bila kufuata taratibu kutoka nchi za ukanda wa maziwa makuu hivyo polisi inatoa muda wote wanaozimiliki kuzisalimisha.

Katika hatua nyingine kamanda Makungu alisema kuwa polisi mkoa Kigoma imeweza kuendesha mikutano 415 ya jamii ili kutoaa elimu kwa jamii kuhusu utii wa sheria bila shuruti ambapo watu 63,404 waliweza kupewa elimu kupitia mikutano hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI