Header Ads Widget

KIMEI AJITOKEZA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA WAPIGAKURA SERIKALI ZA MITAA KITONGOJINI KWAKE



NA WILLIUM PAUL, MOSHI.


Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Stephen Kimei mapema leo asubuhi amejitokeza kujiandikisha katika daftari la wapigakura uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye kitongoji chake cha Mrocha, kijiji cha Komakundi, kata ya Mamba Kaskazini. 



Dkt Kimei amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa  ili  kupata fursa ya kushiriki kuwachagua viongozi wa vitongoji na vijiji katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu. 



Ikiwa ni siku ya kwanza ya zoezi la uandikishaji wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu, wananchi wengi wamejitokeza leo katika Kitongoji cha Mrocha kujiandikisha. 



'Uchaguzi Serikali za Mitaa, Sauti za Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi'


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI