Header Ads Widget

WANAPAWAGA MNA DENI KWA RAIS SAMIA” WAZIRI LUKUVI

 


Na Edwin Dugange

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu na Mbunge wa Jimbo la Ismani, William Lukuvi, Amesema Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ameonesha Upendo kwa Vitendo kwa Wananchi wa Tarafa ya Pawaga.

Waziri Lukuvi Amesema Hayo Wakati wa Ziara Zake za Kukagua Miradi ya Maendeleo ya Kata za Tarafa ya Pawaga Pamoja na Kuzungumza na Wananchi wa Ismani Ambapo Pia Amewasilisha Salamu za Rais kwa Wananchi wa Pawaga.

Lukuvi Amesema Upendo wa Vitendo wa Rais Dkt. Samia kwa Tarafa ya Pawaga Unatokana na Miradi ya Afya, Elimu, Kilimo, Maji na Barabara Inayotekelezwa na Serikali Katika Tarafa Hiyo Wenye Thamani ya Zaidi ya Shilingi Bilioni 60.


Mbunge Lukuvi Amesema Wanapawaga Wana Deni kwa Rais Dkt. Samia la Kumchagua kwa Kishindo Katika Uchaguzi Mkuu 2025 na Kumheshimisha kwa Kuwachagua Viongozi wa CCM Katika Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024.

Miongoni mwa Miradi Aliyoikagua Mbunge Lukuvi Katika Ziara Hiyo Iliyoanza September 28, 2024 ni Skimu ya Umwagiliaji ya Mkombozi Itakayohudumia Kata Tatu za Mboliboli, Itunundu Pamoja na Mlenge Yenye Thamani ya Bilioni 55.

Katika Upande wa Miradi ya Afya, Lukuvi Ametembelea Vituo vya Afya Viwili vya Kata za Ilolompya na Mlenge Pamoja na Zahanati Tatu za Vijiji vya Ukwega, Magombwe na Mboliboli Ambapo Amekagua Utekelezaji wa Miradi Hiyo.

Baadhi ya Miradi ya Sekta ya Elimu Iliyokaguliwa Wakati wa Ziara Hiyo ni Ujenzi wa Shule Mbili za Msingi za Kinyika B na Mkombilenga, Sambamba na Ujenzi wa Bweni la Wavulana Katika Shule ya Sekondari William Lukuvi.

Miradi Mingine ni Ujenzi wa Mabweni Mawili ya Wasichana Sekondari ya Pawaga, Madarasa Manne Sekondari ya Kimande, Mabweni Mawili Sekondari ya Mboliboli na Jengo la Utawala, Maktaba na Kompyuta Sekondari ya Mlenge.

Aidha Mbunge Lukuvi Amekagua Ujenzi wa Barabara kwa Kiwango cha Lami Kutoka Pawaga – Izazi Yenye Urefu wa Kilomita 25, Barabara Hiyo Inatarajia Kurahisisha Usafirishaji wa Mazao Kutoka Pawaga Kwenda Jijini Dodoma.

Ziara ya Mbunge Lukuvi Pia Imehusisha Utoaji Zawadi ya Mitungi ya Gesi kwa Washindi wa Kwanza Hadi wa Tatu wa Mashindano ya Mpira wa Miguu ya CCM CUP 2024 Yaliyokamilika Karibuni Katika Baadhi ya Kata za Tarafa ya Pawaga.

Mitungi ya Gesi 330 Yenye Thamani ya Shilingi Milioni 15 Imetolewa na Mbunge Lukuvi kwa Washindi wa Kwanza Hadi wa Tatu wa CCM CUP 2024, Kila Kata Iliyotembelewa Imepata Mitungi 81 Ili Kuhamasisha Nishati Safi ya Kupikia.

Mashindano ya CCM CUP 2024 Yaliyofanyika kwa Kata Zote 13 za Jimbo la Ismani Yakidhaminiwa na Mbunge William Lukuvi Yanametumika Kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, Kampeni Iliyoanzishwa na Rais Samia.

Wakati wa Ziara Hiyo Lukuvi Amefanya Mikutano ya Hadhara 14 Katika Tarafa Hiyo ya Pawaga Akiwaeleza Wapiga Kura Wake Kuhusu Miradi Iliyotekelezwa na Kuwahamaisha Kushiriki Shughuli za Maendeleo Ili Kufanikisha Miradi Hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI