Na Ashrack Miraji, Matukio Daima App. Tanga
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Mhandisi Juma Hamisini, ametangaza kuongeza milioni 1 kwa washindi wa Shindano la Samia Challenge, akielezea hatua hiyo kama mchango wake binafsi.
Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha shindano hilo, iliyofanyika Oktoba 26 mwaka huu kwenye ukumbi wa Samia, Kange, Tanga, Mhandisi Hamisini alisema, “Niwapongeze kwa ubunifu huu mzuri. Nitawaongeza kwenye mshahara wangu milioni 1 kama mchango. Siku ya Alhamisi, mtafika kwa DC kuchukua vijana wawili waliokuwa wakijifunza mambo ya kitaifa.”
Shindano hili lililoandaliwa na African Anti-Violence Journalist, liliwakutanisha wadau mbalimbali, ikiwemo Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha, na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Abdurhaman Shillow.
Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa shindano hili ni mwanzo mzuri na mwaka 2025 litakuwa bora zaidi. “Tunahakikisha tunatekeleza ilani ya wilaya ya Tanga na kuwaonyesha wananchi mambo yote yanayoendelea.”
Aidha, Mhandisi Hamisini aliahidi kusaidia vijana wanaosoma hadi watakapomaliza shule, akiongeza, “Tutawapa zawadi zaidi; mshindi wa kwanza atapata laki mbili na wa pili laki moja.”
0 Comments