Header Ads Widget

AZAM MEDIA YAZINDUA KAMPENI MAALUM YA 'MENU IMEKAMILIKA'

 



Na Elizabeth Cornely 

KAMPUNI ya Azam Media Group imezindua kampeni maalumu inayojulikana kama 'MENU IMEKAMILIKA'.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo, Meneja Mawasiliano na Mahusiao wa Azam Media, Christinah Korosso, amesema kupitia kampeni hiyo wanalenga kuboresha zaidi huduma kwa wateja wao.

Amesema miongoni mwa maboresho hao ni pamoja na kuhakikisha wateja wake wanapata ufikikaji wa maudhui ya kiwango cha juu zaidi.

"Na kampeni yetu hii maarufu kama Menu Imekamilika, itaboreshwa zaidi kwa kuhakikisha inaonyesha kila kitu kuanzia michezo, tamthilia, mfululizo wa vipindi na chaneli za watoto," amesema Christinah.

Grolia Chuwa ni Meneja Masoko wa Azam Media, amesema kwa sasa maboresho mengine wanayolenga ni kwenye michezo hususani ligi za La Liga Bundesliga, NBC na nyinginezo.

 "Kwa hiyo tunawaomba Watanzania wategemee kupata vitu vizuri katika maeneo mengi lengo ni kuona kwamba kila kundi kwenye jamii ndani nchi yetu  inapata kila hitaji lake kutoka katika vyombo vyetu vya habari,"anasema Gloria.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI