Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP.
TAASISI ya Zanzibar maisha bora Foundation (ZMBF) imetakiwa kuchukua hatua maalumu za kudhibiti maradhi ya kuambukiza yanayowapata akina Mama wajawazito na Watoto.
Rai hiyo imetolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar,Msarifu na Mwenyekiti wa bodi ya Wadhamini ya ( ZMBF) Mhe. Mama Mariam Mwinyi wakati akifungua kongamano hilo.
Mhe.Mama Mariam Mwinyi amesema , juhudi hizo zinalenga kuhakikisha Ustawi wa Mama na mtoto na Udhibiti wa changamoto wanazokabiloana nazo,ikiwemo Ukimwi,kifua kikuu na utapia mlo.
Mama Marian Mwinyi ameyasema hayo tarehe 08 Oktoba 2024 hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege ,Mkoa wa mjini Magharibi wakati akifungua kongamano hilo.
Kongamano hilo ni maalumu kujadili masuala ya afya ya mama mtoto hususani Udhibiti wa maradhi ya TB,HIV na Malaria linalowashirikisha Wataalamu wa afya ya mama na mtoto kutoka Kenya , Nigeria, Tanzania na Skuli ya dawa za Kitropiki ya Uingereza .
Aidha Mhe.Mama Mariam Mwinyi amesema Zanzibar miongoni mwa Nchi za Kusini Jangwa la Sahara na zenye idadi kubwa ya akina mama wanaojifungua .
" Juhudi za pamoja za Wadau na mashirika ya Kimataifa zinahitajika kulipa kipaumbrlele suala la ustawi wa mama Wajawazito na Watoto." Alisema Mhe.Mama Mariam Mwinyi.
Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Afya inashirikiana na Taasisi ya Zanzibar maisha bora Foundation ( ZMBF) na kwamba wataendeleza programu tofauti ambazo tayari zimeanza kuleta mafanikio ya kunusuru maisha ya mama na mtoto ili kufikia malengo yaliyomo kwenye Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2025 na Ile ya Dunia ya 2030.
Aidha Mhe.Mama Mariam Mwinyi ametoa wito kwa Jamii ,za Kimataifa kuendeleza juhudi za pamoja kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa kwa kila mdau kutimiza wajibu wake.
Alisema iwapo dhamira ya kuwajengea Mazingira bora kina Mama wakati wa ujauzito ,kijifungua na kuwa na uhakika maisha ya mtoto anayezaliwa yatakuwa salama.
Kongamano hilo la siku tatu litahutimishwa kwa kutolewa ripoti ya miaka mitano ya Mradi wa Udhibiti wa Afya ya mama na mtoto na kumkinga na maradhi ya TB, Ukimwi na Malaria.
0 Comments