Header Ads Widget

ADEM KUWAPIGA MSASA WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI MKOA WA LINDI

 


Na Hadija Omary 


Wakala wa Maendeleo ya usimamizi wa Elimu (ADEM) kupitia Mradi wa boost wamewajengea uwezo walimu wakuu 554 juu ya uongozi, usimamizi na uendeshaji wa shule kutoka Katika Wilaya tano za Mkoa wa Lindi 


Akifungua Mafunzo hayo kwa Ngazi ya Mkoa yaliyofanyika huko Katika kijiji cha nyangao halmashauri ya Mtama Afisa elimu wa mkoa wa Lindi Joseph mabeyo amewataka walimu hao kwenda kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa Mtaala ulioboreshwa ili Mkoa huo upate mafanikio makubwa katika ufundishaji na ujifunzaji shuleni.


Mratibu wa Mafunzo hayo kituo cha nyangao yacob Abeid Amesema Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tatu Katika Wilaya tofauti za Mkoa huo na kwamba Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo walimu wakuu katika nyanja za uongozi, usimamizi na uendeshaji fanisi wa shule utawala bora katika mamlaka za Serikali za Mitaa 


Baadhi ya walimu wakuu wamesema Mafunzo hayo ni muhimu kwao kwani yanawakumbusha maswala mbalimbali 


Hii ni awamu ya tatu ya mafunzo hayo ambayo yatafanyika katika Mikoa 13 ya Tanzania Bara ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Lindi ikihusisha jumla ya Walimu Wakuu 8,551





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI