Header Ads Widget

HOSPITALI YA NKINGA YAANZA KUTOA HUDUMA ZA UPASUAJI KIBINGWA BILA KUACHA KIDONDA KWA MGONJWA.

 


Mganga Mfawizi wa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga, Dkt. Tito Chaula akizungumza na Matukio Daima app juu ya uanzishwaji wa huduma ya kibingwa na bobezi ya upasuaji bila kuacha kidonda kwa mgonjwa iliyoanzishwa wiki hii.


Na Lubango Mashauri, Nkinga. 


HOSPITALI ya Rufaa ya Nkinga iliyopo  Kijiji cha Nkinga, Kata ya Nkinga, Wilayani Igunga, Mkoani Tabora imeendelea kujizatiti katika uboreshaji wa huduma za kibingwa baada ya kuanzisha huduma mpya kupitia Idara ya upasuaji.


Huduma hiyo mpya ambayo imeanzishwa wiki hii ya kisasa inahusu uchunguzi na upasuaji wa kibingwa bila kuacha kidonda katika magonjwa ya mfumo wa mkojo na figo.


Hayo yamebainishwa leo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga, Dkt.Tito Chaula ambapo amesema kuwa, uanzishwaji wa huduma hiyo ni muendelezo wa kuwasogezea karibu huduma Wananchi za kibingwa na bobezi.


Kwa upande wake Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya mfumo wa mkojo (Urologist) na msimamizi wa kitengo hicho, Dkt.Geofrey Chiloleti  amebainisha aina ya magonjwa watakayoshughulika nayo.


" Watu wenye changamoto za Tezi Dume wataweza kufanyiwa upasuaji bila kuacha kidonda kutokana na kuwepo kwa vifaa hivyo vya kisasa zaidi," amesema Dkt. Chiloleti. 


Ameendele kusema kuwa, matibabu mengine ni kuondoa uvimbe kwenye kibofu cha mkojo (TURBT), kuondoa makovu kwenye uume (Direct vision urethrotomy), upasuaji wa mawe kwenye kibofu (Cystolitholapaxy). 


Huduma nyingine ni uchunguzi wa mirija ya mkojo na figo (Ureterorenoscopy), kutoa vinyama au valve kwenye njia ya mkojo kwa watoto (PUV ablation).


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI