Header Ads Widget

WAZEE WAIOMBA SERIKALI KUSAMEHEWA KODIE ZA MAJENNGO AMBAZO SIO ZA BIASHARA

 


Na  Matukio Daima Media App,Mbeya


WAZEE Jijini Mbeya wameiomba serikali kusamehe  kodi za majengo ambayo sio za biashara kutokana na baadhi yao kuwa  na hali duni za maisha ambazo zinasababisha kushindwa kumudu kulipa na  kupelekea kuwa na malimbikizo ya madeni.


Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 3,2024 na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Mbeya ,Hezron Kapwela wakati akizungumza na mwandishi wa habari kuelekea siku ya wazee Duniani ambayo ufanyika kila Oktoba Mosi kila mwaka.



Amesema  malipo ya kodi za majengo imekuwa kero kwa wazee wasiojiweza na kuomba serikali kuliangalia upya ili kuweza kuwasaidia kwani  idadi  kubwa wanaoishi  mazingira magumu .


 “Kuelekea maadhimisho ya siku ya wazee duniani  tunaomba serikali na wawakilishi wetu bungeni kusamehe kodi za majengo ambazo si za biashara unakuta mzee amejenga nyumba yake  anaishi lakini anakwata kodi anaponunua nishati ya  za umeme suala hili limekuwa ni kero “amesema.


Ameongeza kuwa “Kila wanapofanya mikutano wazee wanalalamika na hatua inayotumika kuandika barua Mamlaka ya mapato ni ndefu na ni gharama  kwa mzee anayeishi kijijini kutokana wengi wao  umri kuwa mkubwa kupata fedha ni tatizo  hivyo tunaomba serikali izingatie”amesema mzee Kapwela.


Kuhusu vijana wanaotelekeza wazazi wao na kuwaachia mzigo wa kulea wajukuu wameombwa itungwe sheria ya kuwabana ili  kuwatunza huku   asilimia kubwa ya  wanaoishi vijijini wanakaa na wajukuu hivyo ni serikali iangalia suala hili na kupitisha sheria bungeni ili iendelee kupunguza matatizo kwa Tanzania kuelekea 2030.


Wakati huo huo ameomba kuingizwa kwenye vyombo vya uwakilishi na kuwa wajumbe halali ili kujadili ukatili wanaofanyiwa  dhidi yao  wa kuporwa mashamba , mifugo, mazao yaliyolimwa ambayo  uporwa na vijana bila kuwashirikisha wazazi ,pamoja na kuomba kuwa na mwakilishi wa wazee bungeni ambaye atazungumza mambo ya wazee.


Kwa upande wake Katibu Baraza la ushauri la wazee Mkoa wa Mbeya ,Said Mwapongo amesema serikali ikatunga sheria sera iliyopo imetungwa 2003, na kwamba sera hiyo ipo zaidi ya miaka 20,bado sheria haitungwi na ni muda mrefu ambayo haitoi matumaini kwa wazee  .


Amesema sheria  waliotunga sera hiyo hawapo kwenye uhai na waliopo kwenye uhai wakaona sheria ya wazee ,lakini  wapo wazee waliotumikia Taifa kwa muda mrefu kwa shughuli zao mbali mbali  huku wengi  hawana uwezo wanaishi maisha ya chini  ni vema  serikali ikaanzisha pensheni kwa wazee kwa ajili ya kuendesha kwa ajili ya kujikimu kama ilivyo Zanzibar .


Aidha Mwapongo amesema kanuni mpya za bima ya afya zikumbuke  kundi la wazee ambao wanapatiwa matibabu bila malipo kwenye vituo vya afya na Zahanati na kwamba bahati mbaya magonjwa yaliyo mengi hayatibiwi kwenye hospitali za wilaya, mkoa pamoja na Rufaa ambapo bima walizonazo haziwezi kufanya kazi ni vema Taifa ikaendelea kuimarisha na kuzitungia kanuni mpya kwa bima walinazo ili ziweze kutumika kwenye hospitali za wilaya ,mkoa na kanda.


Akielezea zaidi Mwapongo wamesema idara ya ustawi wa jamii izidi kujipambanusa ili wazee waweze kunufaika kupitia idara hiyo kwa kuwa idara inayojitegemea  na kuwa na bajeti zake ili wazee wanufaike ,pamoja na sera ya Taifa ya wazee 2003/2019 itungiwe sheria kutokana na sheria iliyopo kuwa ya muda mrefu.


Kwa upande wake Afisa Ufwatiliaji  wa shirika la( RADO )ambalo linajishughulisha na masuala ya wazee ,Musa Mcharo amesema kuelekea siku ya wazee ameikumbusha serikali  Serikali kuendelea kulikumbuka kundi la Wazee hasa wale waishiyo pembezoni Vijijini kwa kuwaboreshea huduma za msingi.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI