Header Ads Widget

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YAMETAKIWA KUWA NA UWAZI NA UWAJIBIKAJI KATIKA SHUGHULI WANAZOZIFANYA.

 



halmashauri ya wilaya ya Nkasi Septemba,03,2024 imefanya mkutano wa mwaka na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wilayani humo.


Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Nkasi Kasimu Abdul Ibrahim amezipongeza asasi za kiraia kwa kuendelea kusaidia serikali katika SHUGHULI za maendeleo huku akivitaka vyombo hivyo kuwa na Uwazi na Uwajibikaji katika miradi wanayoitekeleza ndani ya halmashauri.


Hata hivyo kaimu mkurugenzi halmashauri ya Nkasi Ajaye Abnel Nguvila ameziomba Asasi za kiraia kuendelea kushikiana na serikali pamoja na jamii wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuhamasisha jamii katika uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura.


Kwa upande wake Victor Makoba Mratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ameeleza lengo la mkutano huo wa mwaka ni kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi na kupeleka manufaa makubwa kwa jamii.


Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Nkasi Slemu Mgaya ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kufuata kanuni na taratibu za matumizi ya fedha zinazotolewa na wafadhili ili kuendelea kuaminika na wafadhili na kuondoa mianya ya Rushwa katika utekelezaji wa miradi ndani ya halmashauri

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI