Header Ads Widget

KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 7



Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Lindi Septemba 03, 2024 imemuhukumu Hassan Saddi, mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa Mchinga kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha Jela na kumlipa muhanga fidia ya shilingi laki tano kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka saba mwanafunzi wa darasa la kwanza.


Mtuhumiwa ambaye ni mwalimu wa kujitolea kwenye shule ya msingi Mchinga alitenda kosa hilo Mei 19, 2024 majira ya saa kumi na moja na dakika ishirini jioni huko katika kijiji cha Mchinga wilaya ya Lindi baada ya kumrubuni kwa kumuonyesha picha za ngono nyumbani kwake kisha kumbaka.


Mtuhumiwa huyo baada ya kutekeleza uovu wake huyo alikimbia mpaka alipokamatwa Juni 10, 2024 na kufikishwa mahakamani kisha kusomewa shitka linalomkabili.


Hukumu hiyo ya kesi namba 15710 ya mwaka 2024 imetolewa na hakimu mkazi wa mahakama hiyo Mhe. Delphina Kimath huku upande wa mashtaka  ukiongozwa na John Remy na Hadija Mwambungu ambapo jumla ya mashahidi sita upande wa Jamhuri walitoa ushahidi pamoja na vielelezo viwili.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI