Header Ads Widget

MIKOPO NMB YAWAINUA KIUCHUMI WALIMU UVINZA

 


Walimu wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya wilaya Uvinza wakiwa katika semina ya siku maalum ya walimu iliyoandaliwa na benki ya NMB kwa ajili ya kukutana na walimu hao kutoa elimu na kutangaza masuluhisho ya huduma za kifedha yanayotolewa na benki hiyo.
 

Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Magharibi Restus Assenga akizungumza katika seminaya  benki hiyo na walimu wa shule za Msingi na Sekondari katika halmashauri ya wilaya Uvinza Maarufu kama Teacher’s Day unaoendelea nchini kueleza huduma za kifedha zinazoweza kuinua Maisha ya walimu hao kiuchumi.

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

IMEELEZWA kuwa mikopo  inayotolewa na benki ya NMB kwa walimu na watumishi wa halmashauri ya wilaya Uvinza imewezesha walimu hao kuanzisha miradi ya kiuchumi na kuboresha Maisha yao hali iliyofanya watumishi wengi kuendelea kufanya kazi na halmashauri hiyo badala ya kukimbia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Uvinza, Fred Millanzi alisema hayo akifungua semina ya siku moja kwa walimu wa shule za msingi na sekondari wa halmashauri hiyo iliyoandaliwa na benki ya NMB ili kutoa suluhisho la huduma za kifedha zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo mikopo.

Millanzi alisema kuwa taarifa aliyonayo inaonyesha kuwa idadi kubwa ya watumishi hao wanapitishia mishahara yao katika benki hiyo lakini wamekuwa wakitumia huduma mbalimbali za benki hiyo ikiwemo mikopo ambayo imechangia walimu hao na watumishi wengine kushughulikia masuala mbalimbali ya kifamilia na kiuchumi.

Kwa upande wake Afisa utumishi wa halmashauri hiyo ya wilaya Uvinza alisema kuwa fursa ya mikopo kwa watumishi wa umma wanapokuwa kwenye utumishi ni muhimu kwa ajili ya kuwaandalia Maisha yao ya baadaye kwa kuanzisha miradi ambayo itakuwa ndiyo ngao yao baada ya  kustaafu.

Awali Meneja wa kanda ya Magharibi wa benki ya NMB, Restus Assenga akizungumza katika semina ya  benki hiyo na walimu wa shule za Msingi na Sekondari katika halmashauri ya wilaya Uvinza alisema kuwa semina hiyo imelenga kutoa elimu ya fedha kwa wlimu hao lakini kutangaza fursa za masuluhisho ya huduma za fedha ambazo zinapatikana katika matawi ya benki hiyo.

Assenga alisema kuwa walimu ni moja ya wateja wao muhimu katika utumishi wa umma ingawa bado wengi wao hawajafikia masuluhisho ya huduma za fedha wanazotoa hivyo kuitisha mikutano hiyo kutoa uelewa wa namna walimu hao wanaweza kutumia fersa hiyo kutumia huduma zao za mikopo kuwawezesha walimu kuanzisha miradi ya kiuchumi.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI