Header Ads Widget

THBUB YATOA RAI KWA JAMII KUACHA KUNICHUKULIA SHERIA MKONONI






Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima App Dodoma

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ( THBUB ) imezidua gari lenyethamani ya zaidi shilingi Milioni 300 huku wakitoa rai kwa jamii kuacha kunichukulia sheria Mkononi. 

Akiongea Mara baada ya uzinduzi wa gari hilo Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za binadamu na Utawala Bora Mathew Mwaimu amesema kumekuwepo na matukio mengi ya watu kujichukulia sheria mkononi jambo ambalo sio zuri. 

"Ni wazi kuwa watanzaniania tunako endelea siko kwa sababu nchi ya Tanzania ni nchi ya kistarabu na ustarabu huu ndio unaotutaka kufanya kila jambo kuzingatia sheria, " Amesema. 

Na kuongeza "Tunazungimzia Tanzania nchi inayopaswa kufuata utawala wa sheria hivyo kwa lolote linalotokea mtu ni wazi kila mmoja  anapaswa kuhakikisha kwamba anapona jambo la hatari anapaswa kutoa taarifa katika vyombo stahili na vyombo hivyo vitaweza kuchukua hatua zinazostahili, " Amesema Jaji Mwaimu. 

Amesema sio jambo jema kuondoa uhai wa mtu bila kufuata utaratibu wa kisheria.




Aidha akizungumzia gari hilo amesema uzinduzi wa basi hilo litawasaidia namna ya kuwafikisha watumishi wa Tume katika maeneo yao ya kazi na kupunguza gharama za usafiri. 

" Gari hili linakwenda kusaidia katika utendaji kazi hasa pale tutakapokuwa tunasafiri mikoani kwasababu moja ya shughuli za Tume nikutoka nje ya ofisi kwaajili ya kufanya uchunguzi, kutoa elimu kwa umma, na kwenda kufanya tafiti hivyo gari hili linakwenda kusaidia kazi nyingine nyingi zinazotekelezwa na Tume, " Amesema

Kwa upande wake Katibu Mkuu wizara ya Katiba na Sheria  Eliakim Maswi
amesema basi hilo limenunuliwa kwa fedha za ndani kwamaana ya serikali imetoa pesa ili linunuliwe basi kwaajili ya kutoa huduma kwa watumishi wa tume.

"Tume hii ni moja wapo ya tume muhimu Sana ya ndani ya serikali yetu ambayo inasimamia Haki za binadamu, " Amesema Katibu Mkuu huyo. 

Ameeleza katika kuwawezesha kufanyakazi vizuri serikali ikaona  kuna umuhimu wa tume kuwa na chombo chake cha usafiri kitakachowasaidia watumishi wake katika utumishi wake wa umma. 

"Umuhimu wa tume hii ambayo inatuangalia Sisi kama watanzania na shughuli zetu tunazofanya na inatambulika kimataifa kwaajili ya Haki za binadamu ndani ya nchi, "Amesema Katibu Mkuu huyo Maswi. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI