Header Ads Widget

TAKUKURU YAWAFUMBUA MACHO WANANCHI,WASEMA WAGOMBEA WATOA RUSHWA HAWANA NAFASI TENA

Thobias Mwanakatwe,SINGIDA 

WANANCHI wamesema elimu waliyopewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa Nchini (TAKUKURU) imewasaidia kuelewa madhala yake hivyo kama kuna wagombea ambao wamejipanga kutoa rushwa wakati wa uchaguzi ni bora wasichukue fomu za kugombea uongozi.

Wakizungumza jana kwenye banda la TAKUKURU katika  maonesho ya saba ya kitaifa ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yakiyohitimishwa jana⁷, walisema katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wagombea wasifanye pesa kama ndio sifa ya kutaka kuchaguliwa.

Mmoja wa wananchi hao Rajabu Nkangu, alisema TAKUKURU imefanya kazi nzuri kuwaelimisha madhala ya rushwa hivyo wagombea ambao kila inapofika wakati wa uchaguzi wanatumia pesa zao kuwahonga wananchi ili wawachague sasa wajipange hawadanganyika tena.

"Wakati wa uchaguzi baadhi ya wagombea wanatumia pesa zao kutuhonga ili tuwachague na viongozi wa namna hii wakishachaguliwa wanakaa mbali na wananchi bila kuleta maendeleo yeyote, sasa tumeamka wenye tabia hiyo bora wasije kuchukua fomu hatutawachagua," alisema.

Naye Godfrey Gunda alisema elimu waliyopewa na TAKUKURU itawasaidia sana wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani ambapo wataitumia kama fimbo ya kuwadhibu wagombea watoa rushwa.

Gunda alisema kuchagua kiongozi mtoa rushwa wamebaini kumekuwa kukiwagharimu sana kutokana na kukaa miaka mitano bila kuletewa maendeleo kwasababu viongozi wanaotoa rushwa wakishachaguliwa wanakuwa hawana habari na wananchi.

Naye Amina Selemani alisema atakuwa balozi kwa wananchi wengine kuwaelimisha madhara yatokanayo na rushwa kwani rushwa inazorotesha maendeleo ya nchi na kuwafanya wananchi kukosa haki za msingi.

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Petro Horombe, alisema katika kipindi cha wiki moja ya maonesho hayo banda lao lilitembelewa na wananchi wengi sana wakiwa viongozi wa vyama vya siasa na watendaji wa serikali.

"Watu wasiopungua 115 wamefika kwenye babda letu ambapo wote waliofika wamenufaika kupata elimu juu ya mapambano dhidi ya rushwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani " alisema Horombe.

Horombe alisema TAKUKURU ilichobaini kwenye maonesho hayo kwa wananchi waliofika katika banda lao wameipenda elimu waliyopewa,wameipokea na wamekubali kutoa ushirikiano kwa taasisi katika kukomesha vitendo vya rushwa nchini.

"Wananchi waliofika katika banda la TAKUKURU tafsiri yake kila mmoja akiwa balozi wa mwenzake akimwelimisha ndugu yake,jirani yake,mtoto wake,mke wake,mume wake na kadhalika maana yake elimu hii itasambaa sana" alisema.

Horombe alisema elimu waliyootoa ni ya msingi sana kwani ni sehemu ya uzuiaji rushwa na wananchi wanapokuwa wameelimika juu ya madhala ya rushwa watajua thamani ya kura wanayopiga wakati wa uchaguzi.

"Wananchi  wakielimika watakuwa wanajua hatma ya yake ya maendeleo ipo katika ile kura anayokwenda kuipiga na sisi tunakuwa na uhakika wananchi wanakwenda kufanya maamuzi kupitia kura yao na wanatambua thamani ya kura yao," alisema.

Horombe alisema wamewasisitizia wananchi waliofika katika banda la TAKUKURU kwamba siku ya uchaguzi watambue baada ya watakayopiga wana miaka mitano ya kukaa na kiongozi waliyomchagua na dirisha jingine litafungiliwa baada ya miaka mitano hivyo wasifanye kosa maana ni kipindi kirefu sana.

Maonesho ya saba ya kitaifa ya Mifuko ya Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yalianza mjini Singida Septemba 8 na kuhitimishwa Septemba 14 mwaka huu.

MWISHOTAKUKURU YAWAFUMBUA MACHO WANANCHI,WASEMA WAGONBEA WATOA RUSHWA HAWANA NAFASI TENA 

MWISHO

Post a Comment

0 Comments

MAGAZETI

NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI