Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imemuhukumu kifungo cha maisha jela, Fumo Renatus (26) Mkazi wa Migoli Mkoani humo kwa kosa la kumbaka Mtoto mwenye umri wa miaka 9 .
Mtuhumiwa Fumo Renatus alikuwa akimlaghai na kumdanganya Mtoto huyo na kwenda nae kwenye kichochoro na kumuingizia vidole Binti huyo sehemu zake za siri , na siku ya tukio akiwa na Mtoto huyo alimuingilia kwa kumuingizia uume wake sehemu za siri na alipomaliza alimpatia fedha kiasi cha shilingi mia tano huku akimtisha asiseme na akisema atamfanya kitu kibaya.
Kesi hiyo ya jinai Imesikilizwa leo September 26,2024 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Honorious Kando ikiwa na jumla ya Mashahidi watatu akiwemo Mhanga wa tukio ambaye ni Mtoto huyo, Mama mzazi pamoja na Daktari.
Hata hivyo Mama mzazi wa Binti huyo aliiambia Mahakama kuwa alibaini utofauti kwa Mtoto wake kwa kutembea huku akichechemea na alipomuhoji kwa kumbana Mtoto alimueleza ukweli wote na ndipo Mama mzazi alipofanya maamuzi ya kwenda ofisi ya kijiji na kisha kituo cha Polisi na aliandikiwa fomu ya Polisi namba tatu yaani ( PF3 ) na kisha kumpeleka Hospitali.
Mshtakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea alikana kuhusika na kosa hilo lakini Mahakama kupitia ushahidi uliotolewa ulijiridhisha kuwa ni sahihi alitenda kosa hilo.
0 Comments