Na Lilian Kasenene, Morogoro
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kwa wakulima wa Miwa wa kijiji Cha Luhembe Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro baada ya ekari zaidi ya 1,000 za mashamba ya Miwa kuungua moto.
Ekari za mashamba ya Miwa zaidi ya 1,000 zilizoungua moto ni sawa na tani 30,000 yenye thamani ya sh bilioni 3.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Dennis Londo alitoa salamu za Rais kwa wakulima hao wa miwa baada ya kufika kijijini hapo.
Londo alisema"Rais anawapa pole sana wakulima na ametaka mwekezaji kwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha Miwa ya wakulima inakatwa ili kuondoa hasara ya wakulima na kuondolewa shambani na kuipeleka kiwandani kwa haraka,".
Alisema mwekezaji tayari ameanza kutekeleza maagizo ya Rais na taratibu ya kuondoka Miwa ya wakulima shambani na kuipeleka kiwandani.
Amemshukuru Rais, na mwekezaji kwa kutekeleza maelekezo ya Rais na kuyafanyia kazi kwa haraka kwa kusimamisha shughuli zote za ukataji wa Miwa kawaida na kuelekeza nguvu kwenye kukata Miwa iliyoungua pekee na kupelekwa kiwandani.
....
0 Comments