NA WILLIUM PAUL.
MBUNGE wa Jimbo La Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi amehudhuria kikao cha kikazi kuiwakilisha Tanzania katika mkutano wa kimataifa unaohusisha nchi 54 (Indonesia Africa Parliamentary Forum 2024) jijini Bali, Indonesia.
Lengo kuu la mkutano huo ilikuwa ni kujadiliana namna bora ya kuendeleza mahusiano na ushirikiano katika sekta mbalimbali kwa manufaa ya nchi zetu mbili na bara la Africa kwa ujumla.
Katika picha kutoka Kulia anaonekana Prof. Patrick Alois Ndakidemi Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Jesca David Kishoa Mbunge wa Viti Maalumu, Dkt. Puan Maharani Spika wa Bunge la Indonesia na Zubeir Ali Maulid, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mwisho.
0 Comments