Na, Matukio Daima App,
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amemwambia Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni kwamba jeshi la Polisi haliwezi kujichunguza lenyewe kwenye katika sakata la utekaji.
Mwenyekiti Mbowe, amesisitiza kwa kumtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuunda tume ya kijaji ya kimahakama ambayo itachunguza matukio ya watu kupotea na kuuawa kwa siku za hivi karibuni.
Katika hatua nyingine, Mbowe amesema ndani ya jeshi la polisi kuna watu wema na wahalifu, hivyo, kumtaka Waziri Masauni kuelewa kuwa wananchi wanahasira kutokana na matukio yanayoendelea hapa nchini, na kutaka serikali kuangalia namna ya kurekebisha hasira hiyo.
"Ndani ya jeshi la Polisi kuna watu wema na watu wahalifu, sasa nyinyi mmekubali kuishi na wahalifu hao sasa suluba za wananchi zikitokea muelewe wananchi hao wanahasira, nimesema sasa hasira hii leo ipo hapa huku tunapokwemda kama hamturekebisha hasira hii itakuwa kwa watu barabarani" Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema.
0 Comments