Na, Matukioi Daima App,
Vurugu ziimetokea katika msiba wa aliyekuwa kada wa Chadema, Ali Kibao nyumbani kwake mkoani Tanga, wakati Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni akitaka kuwahutubia wananchi.
Kelele hizo zimeibuka zikimtaka Waziri Masauni kujiuzulu nafasi yake kutokana na matukio ya kutekwa wananchi yanayoendelea nchini kwa sasa.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alifanikiwa kuwatuliza wananchi hao kwa kuwaomba kumuacha Waziri Masauni amalizie hotuba yake.
Aidha katika hotuba yake, Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amemshukuru Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kwa hekima zake pamoja na kufikisha salamu za Rais Samia Suluhu Hassan na kusema kuwa ameumizwa sana na tukio hilo hivyo kuwataka wananchi kuliachia jeshi la polisi kufanya kazi yake.
0 Comments