Header Ads Widget

MTOTO WA MIEZI SITA AFARIKI BAADA YA BABAKE KUMBAKA



Mtoto mwenye Umri wa Miezi Sita amefariki baada ya kubakwa na baba yake Mzazi jana usiku majira ya saa tatu usiku katika eneo la Mbuyuni kata ya Kizota jijini Dodoma.


Bibi wa Marehemu Elizabeti Sudai akieleza tukio hilo amesema baba huyo alimgongea usiku huo na kumuita amchukue Mtoto na alipotoka Nje alikuta mtoto amelazwa chini mlangoni akiwa haonyeshi kuwa hai.


Anasema hakumkuta baba huyo nje hapo hivyo aliamua kumchukua mtoto na kumpeleka kwa balozi na badae kumpeleka hospitali ndipo alipogundulika kuwa alibakwa na ameshafariki.


Mweyekiti wa Shina Mtaa wa Mbuyuni Tausi Rashidi amesema baada ya Mtoto huyo kufikishwa kwake aimtafuta mama wa mtoto ndipo akaeleza baba huyo alikua akicheza na mtoto huyo na kuondoka naye Muda wa saa Moja Usiku hakurejea hadi muda huo alioenda kwa balozi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma George Katabazi akitoa taarifa ya tukio hilo amesema mtuhumiwa ambaye ni baba wa Mtoto amekamatwa na jeshi hilo linaendelea na uchunguzi Zaidi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI