Header Ads Widget

MPANGO WA RAISI SAMIA KUMTUA MAMA NDOO WASHIKA KASI

 



Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Godfrey Mnzava (katikati) akifungua bomba la maji ikiwa ishara ya kuzindua upatikanaji wa maji safi na salama katika kijiji cha Nyamnyusi Halmashauri ya wilaya Kasulu mkoani Kigoma ambapo watu 10,000 watanufaika na mradi huo

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MPANGO wa Raisi Samia Suluhu Hassan wa kumtua mama ndoo unazidi kushika kasi baada ya serikali kukamilisha mradi mkubwa wa maji wenye gharama ya shilingi Bilioni katika Kijiji cha katika halmashauri ya wilaya Kasulu mkoani Kigoma.

 

Akizungumza baada ya kuzindua mradi huo wa maji Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Godfrey Mnzava alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni matokeo ya dhamira ya dhati ya Raisi Samia katika kuondoa adha kwa wananchi kufuata maji umbali mrefu.

 

Kutokana na hali hiyo Mnzava ametaka wananchi kulinda vyanzo vya maji visiharibiwe wala kuchafuliwa sambamba na kutaka kulindwa na kutunzwa kwa miundo mbinu ya maji inayotumika kufikisha huduma kwa wananchi.

 


Akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge Meneja wa Wakala wa maji mijini na vijijini (RUWASA), Mhandisi  alisema kuwa jumla ya shilingi Bilioni 1.6 zimetumika kutekeleza mradi huo zikihusisha ujenzi wa chanzo cha maji na ujenzi wa tanki litakalobeba lita 225,000 huku watu 10,000 wafaidika na mradi huo.

 

Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Diwani wa kata ya alisema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuweza kukamilisha mradi huo hivyo kufikisha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.

 


Meneja wa RUWASA wilaya Kasulu Edward Kisalu (kushoto) akitoa maelezo kwa viongozi wa mbio za mwenge kuhusu mradi wa maji Nyamnyusi

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI