Header Ads Widget

MNYAMA SIMBA ASHAMBULIA MIFUGO KIJIJI CHA LUMULI .

 


Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP Iringa.

MIFUGO kadhaa imeshambuliwa na kuliwa na mnyama anayesadikiwa kuwa ni Simba mla Watu,ambapo tahadhari imetolewa na kwa Wananchi wa eneo hilo kuchukua tahadhari.              



Mhe.Yohanesi Mlusi wa Kata ya Lumuli Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini ametoa Wito huo wakati wa ibada ya mazishi ya Mwananchi mmoja wa Kijiji cha Muwimbi.


Mhe.Mlusi alisema amepokea taarifa za uhalifu uliofanywa na mnyama huyo anayesadikiwa kuwa ni mnyama Simba kutoka kwa Wananchi waliofikwa na Janga hilo.                 


"Taarifa niliyoipata ni kwamba Mbuzi Wawili wamepotea na ng'ombe mmoja pamoja na mifugo mingene wakiwepo kuku na Mbwa".Alisema Mhe.Mlusi.                  


Alisema kufuatia sintofahamu hiyo aliamua kutoa taarifa kwa Uongozi wa Serikali ngazi ya Wilaya kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini ili kupata msaada wa haraka kutoka TANAPA.                    


Hata hivyo baada ya kupata taarifa na kuzifikisha Septemba 06 /2024 Kuna mzoga wa ng'ombe umepatikana ukingoni mwa mto sehemu ambayo awali kulioneka nyayo za mnyama huyo.     

Awali Bw. Elick Ng'eng'ena alitoa taarifa za ng'ombe wake kupotea katika mazingira ya kutatanishwa,na ilikuwa ni baada ya jirani yake kudai Mbuzi wake Wawili kupotea na mmoja kukutwa kicha bila kiwiliwili.


Bw.Ng'eng'ena alisema pamoja na kutoa taarifa kwa Viongozi ambao walifika kujiridhisha na madai ya kuwepo kwa nyayo za mnyama Simba naye aliendelea na ufuatiliaji wake binafsi.   


" Baada ya Uongozi kwenda Halmashauri Mimi niliamua kutongoja uchunguzi wao niliamua kuvalia nyuga na kisha kugundua mzoga wa ng'ombe wangu mita chache kutoka pale tulipokuwa kukagua nyayo za mnyama huyo."Alisema Bw . Ng'eng'ena

Mwananchi mwingine Agrey Televa alidai kuwa Mbuzi wake Wawili walidaiwa kupotae aligundua mabaki ya kichwa kimoja cha mbuzi bila kuona mzoga.


Aidha  Bw.Daud Ngogo alisema eneo hilo miaka ya 54 ilikuwa ni makazi ya Mkulima wa Tumbaku aliyejukana kwa jina la Tajiri Hasanari ( Mgiriki) ambaye kwa wakati wake alikuwa akijilinda na Wanyama wakali  kwa silaha za moto .           

Hata hivyo  Bw.Ngogo aliziomba Mamlaka  kuchukua hatua za haraka kabla Kata hiyo haijaingia kwenye majanga.



Picha mbali mbali za ufuatiliaji wa mnyama Simba.


Mzoga wa Ng'ombe.
Unyayo unaodaiwa kuwa ni wa mnyama Simba.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI