Header Ads Widget

MBOWE, LISSU WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI

Na, Matukio daima App,

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe amekamatwa na Polisi eneo la Magomeni, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 23, 2024.

Kabla ya Mbowe kukamatwa, alifika eneo hilo akiwa na gari dogo, kisha kuanza kuzungumza na waandishi wa habari kama ishara ya kuajianda na maandamano.

Itakumbukwa, Septemba 11, 2024, Mbowe alitangaza kufanyika maandamano ya kulaani matukio ya watu kutekwa na mauaji, akiwemo kada wake, Ali Kibao. Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilitangaza kuyapiga marufuku maandamano hayo.

Kwa mujibu wa Mbowe, wameamua kuweka mkazo suala hilo, baada ya maombi ya mahitaji, ikiwemo kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama kama sehemu ya uwajibikaji.

Amesema jambo lingine waliloliomba ni kurejeshewa kwa viongozi wa chama hicho, waliotekwa kwa nyakati tofauti wakiwa hai au hali ya umauti, akiwemo Deusdetith Soka, Dioniz Kipanya, Jacob Mlay na Mbwana Kombo.

Huku Mwenyekiti Mbowe akikamatwa Magomeni, Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu amesema Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu amekamatwa na polisi asubuhi ya leo jumatatu nyumbani kwake saa chache kabla ya kuanza kwa maandamano.

“Lissu amekamatwa nyumbani kwake Tegeta na amepelekwa Kituo cha Polisi Mbweni na mimi kama wakili niko njiani nakwenda huko kujua sababu za kukamatwa kwake,” amesema wakili Hekima.

Aidha taarifa zinadai kuwa mpaka sasa kuna viongozi na wanachama wa chadema ambao idadi yao kamili bado haijafahamika wakekwisha kamatwa na jeshi la polisi kutokana na mandamano waliyoyaitisha ya na kuyapa jina la maombolezo na amani, jijini Dar es Salaam.

TAZAMA TUKIO ZIMA LA KUKAMATWA MBOWE KUPITIA LINK HII

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI