NA MATUKIO DAIMA APP
Mungu ibariki Tanzania,Dumisha uhuru na Umoja,Wake kwa Waume na Watoto ni sehemu tamu zenye kufikirisha katika wimbo wa Taifa amini Maneno haya ukiyaimba Uunajivunia uzalendo mkubwa kwa Taifa letu Tanzania.
Wimbo huu huimbwa rasmi katika hafla za kitaifa, mashindano ya michezo ya kimataifa, na shughuli mbalimbali za kijamii na kisiasa ni ishara ya uzalendo, umoja, na amani kwa Taifa la Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla.
Baadhi ya nchi ulimwenguni Suala la uzalendo kwa Taifa ni kama ibada ya Kila kwa waumini wa dini mbali mbali na ndio maana kamwe hutaona nchi hizo zikieneza taswira mbaya inayochafua nchi yao.
Nchini Tanzania si kwamba uzalendo hakuna lah hasha uzalendo upo ila tafsiri yake kwa baadhi yetu tunafikiri uzalendo ni wa watu furani waliopo serikalini ndio wanatakiwa kuwa wazalendo ila Mimi mtoto wa muokota matunda sipaswi kuwa mzalendo .Kama ilivyokwenye wimbo wa Taifa Maneno yaliyopo Jinsi yanavyohimiza uzalendo ni wazi Kila mmoja kuanza kuimba wimbo huo toka ndani ya sakafu ya Moyo na inapowezekana kuwekeza kueneza uzalendo maana tunajivuna na kufanya shughuli zetu kwa amani kwa sababu tunaishi ndani ya amani iliyoasisiwa na waasisi wa Taifa hili wakiongozwa na baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mungu ailaze roho take mahali pema peponi Amin.
Si kwamba wote hawaoni hawaoni jitihada hizo wapo wanaoona na hata kuendelea kuunga mkono jitihada za kueneza amani ndio maana katika kuunga mkono jitihada hizo mdau wa maendeleo wilayani Kilolo mkoani Iringa Aidan aliamua kuja na bonanza Mlawa Cup 2024.
Mabonanza ya Mlawa Cup yalivyokuza Vipaji, Kukuza Michezo na Kudumisha Uzalendo kwa Vijana Wilayani Kilolo kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.
Hakuna ubishi kuwa michezo ni nyenzo muhimu sana katika kuhamasisha maendeleo ya jamii, kukuza vipaji, na kuimarisha uzalendo miongoni mwa vijana.
Katika muktadha wa wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa, mashindano ya Mlawa Cup yaliyoshirikisha timu zaidi ya 10 yamejizolea umaarufu mkubwa kama mojawapo ya majukwaa muhimu ya michezo.
Mabonanza haya yamekuwa si tu fursa kwa vijana kuonyesha vipaji vyao, bali pia yana umuhimu mkubwa katika kuimarisha mshikamano wa kitaifa, kukuza maadili ya kijamii, na hata kusaidia maandalizi ya chaguzi zijazo.
Mashindano ya Mlawa Cup yameleta mwamko mpya kwa vijana katika wilaya ya Kilolo, kwa kutoa fursa za kipekee kwa wachezaji wachanga kuonyesha uwezo wao wa kimichezo.
Kwa mara ya kwanza, vijana wenye vipaji ambao pengine hawakuwa na jukwaa la kujitambulisha wanapata nafasi ya kuonyesha uwezo wao mbele ya mawakala wa timu za kitaifa, walimu wa michezo, na mashabiki wa ndani na nje ya wilaya.
Mashindano haya yanajumuisha michezo mbalimbali kama vile soka, pia Sanaa mbali mbali ikiwemo ya kumtumia Msanii maarufu wa Sauti ya Hayati Magufuli Baraka Mwakipesile ama Baraka Magufuli kufikisha ujumbe hali inayowafanya vijana kutoka maeneo tofauti ya wilaya hiyo kupata jukwaa la kushindana na wenzao.
Chini ya Mtangazaji nguli wa Kituo Cha Utangazaji Cha Radio Ebony Fm Iringa Edwin Bashir hamasa ilikuwa kubwa na ushindani huu ulikuwa chachu ya kujituma kwa vijana wengi, wakiiona Mlawa Cup kama fursa yao ya dhahabu kupata nafasi ya kuingia katika ligi kubwa za kitaifa.
Kwa mfano, baadhi ya vijana ambao walishiriki katika mabonanza haya tayari wamepata nafasi ya kucheza katika timu za daraja la kwanza nchini Tanzania, huku wengine wakipata ufadhili wa masomo na mafunzo maalum ya michezo.
Mratibu wa bonanza la Mlawa Cup Moshi Kivamba ama Mr Majungu anasema ubunifu wa jambo hilo ni wa kupongezwa, kwani Mlawa Cup imefanikiwa kuziba pengo lililokuwepo kati ya vipaji vya vijana wa vijijini na fursa za kitaifa.
Kuwa hata wale vijana ambao hawakujulikana na jamii yao kwa vipaji vya michezo wameweza kuibuliwa kupitia mashindano haya, na sasa wanajulikana hata kimkoa na kitaifa.
"Mbali na kuibua vipaji, Mlawa Cup pia imechangia kwa kiasi kikubwa katika kuinua hali ya michezo wilayani Kilolo"
Anasema mashindano haya yameleta ari mpya katika shule za msingi, sekondari, na vikundi vya michezo vya mitaani, huku vijana wakiongeza juhudi katika mazoezi na kujituma ili kujiandaa kwa mashindano.
Kwa kuwa michezo ni afya, mashindano haya yamechochea vijana kushiriki kikamilifu katika mazoezi, na hivyo kupunguza changamoto za kiafya kama vile unene uliopitiliza na magonjwa yanayotokana na kutokufanya mazoezi.
Aidha, kutokana na mwitikio mkubwa wa vijana, timu nyingi za michezo wilayani Kilolo zimeanzishwa au kuimarishwa, jambo ambalo limechangia kukuza michezo kwa ujumla.
Mratibu huyu anasema mashindano haya pia yameleta uwiano wa kijinsia katika michezo, kwani yanashirikisha michezo ya wanawake kama vile netiboli.
Kuwa hii imewezesha vijana wa kike kupewa fursa sawa na vijana wa kiume kuonyesha uwezo wao wa kimichezo, hivyo kuvunja vikwazo vya kijinsia vilivyokuwepo. Aidha, wanawake wanapata hamasa ya kushiriki kikamilifu katika michezo na kuwa mfano kwa wasichana wengine.
Alisema Mlawa Cup imekuwa ni chombo muhimu si tu kwa kuendeleza vipaji, bali pia kwa kuinua michezo wilayani Kilolo.
Kuwa na vijana wengi wenye afya bora, walio na ari ya mafanikio, na wanaoishi maisha yenye nidhamu kupitia michezo.
Said Kiponza anasema kuwa akiwa kama mdau wa Michezo anapongeza michezo hiyo kwani ina uwezo wa pekee wa kuleta watu pamoja, hata wale wenye tofauti za kijamii, kiitikadi, au kikabila.
Kuwa hitaji la Vijana Kilolo katika michezo ni kubwa upande wa Vifaa vya michezo na kuwa kupitia mabonanza hayo imekuwa fursa kubwa kwao.
Kuwa Mlawa Cup imekuwa kama daraja la kudumisha umoja na uzalendo miongoni mwa vijana wa wilaya ya Kilolo.
Pia Kiponza anasema mabonanza hayo yameibua mambo mengi kama kupunguza Matukio ya ubakaji , matumizi ya dawa za Kulevya .
Kiponza ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Kilolo anasema mabonanza haya yamehifadhi ushindi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na CCM kwenye Uchaguzi mkuu.
Kuwa vijana kutoka kata mbalimbali, ambao huenda walikuwa na tofauti za kijamii au kiitikadi, wanapata fursa ya kushirikiana na kushindana kwa lengo moja kuleta ushindi kwa timu zao wilaya ya Kilolo.
John Kisia ni mmoja kati ya Vijana wanufaika Mlawa Cup anasema kuwa Mashindano haya yamekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha umoja, kwa kuwa yanafanyika kwa utaratibu wa kushirikisha kata zote za wilaya, na timu zinapangwa kwa uwiano wa pande zote. Hii inawawezesha vijana kutoka maeneo mbalimbali kujenga urafiki, kushirikiana, na kufahamu changamoto wanazopitia wenzao kutoka kata nyingine. Hivyo, Mlawa Cup inachochea vijana kuwa wazalendo na kupunguza migawanyiko ya kikabila au kisiasa ambayo inaweza kusababisha vurugu au mizozo.
Hata hivyo anasema mashindano hayo yam, yameendeshwa kwa uwazi na usawa imekuwa darasa la kufundisha vijana umuhimu wa kuheshimu sheria, nidhamu, na uwajibikaji. Kwa kuzingatia kuwa michezo inahitaji uadilifu, vijana hujifunza kuwa wachezaji wa haki, waaminifu, na wenye nidhamu, sifa ambazo ni muhimu sana katika kujenga jamii yenye mshikamano na uzalendo.
Kuwa Mlawa Cup pia imekuwa na nafasi maalum katika maandalizi ya vijana kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania. Michezo imekuwa nyenzo muhimu katika kutoa elimu ya uraia kwa vijana na kuwafanya wawe na ufahamu wa haki zao za kidemokrasia.
Wakati wa mashindano haya pia elimu juu ya umuhimu wa kushiriki katika chaguzi, kuwa na uchaguzi wa amani, na umuhimu wa kuchagua viongozi bora.
Aidha, kwa kuwa mashindano haya yanashirikisha vijana wengi kutoka kata mbalimbali, yamekuwa kama darasa la kuwafundisha vijana umuhimu wa kushiriki katika mchakato wa uchaguzi na kuwa na mtazamo wa kitaifa badala ya kushikilia mitazamo ya kibinafsi au kikanda.
Vijana wanajifunza kuwa sehemu ya mchakato wa demokrasia kwa kushiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi na pia kuchagua viongozi wanaoamini wanaweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao.
Aidam Mlawa ambae amesomeshwa kwa
pipa la pombe anasema anafanya hayo yote kama sehemu ya kurejesha fadhila kwa wanakilolo lakini kuona serikali ya Chama Cha mapinduzi (CCM) inaendelea kuungwa mkono na Kila mmoja Wetu .
"Ni wajibu wa Kila mtanzania kudumisha amani sehemu alipo kwani amani yetu ni tunu kubwa kwa Taifa na tunafurahia amani kwa kuwa wapo walioipigania hivyo tuienzi "
Anasema kuwa si tu amechangia katika michezo na kuibua vipaji, bali pia imekuwa chombo cha kuwaelimisha vijana kuhusu demokrasia, uzalendo, na umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi.
Kupitia mabonanza haya ya Mlawa CUP 2024 ndipo naiona Thamani ya kuwa mtanzania naona uzalendo unaotembea kwenye Mioyo ya Vijana hawa maana wastani wa watu zaidi 20000 walishiriki mabonanza haya yaliyofanyika zaidi ya miezi miwili ni wazi uzalendo umetembea .
Mashindano ya Mlawa Cup yamekuwa na mchango mkubwa sana katika wilaya ya Kilolo kwa kuibua vipaji, kukuza michezo, kudumisha uzalendo, na kuandaa vijana kuelekea chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.
Pasipo shaka michezo inaweza kutumika kama nyenzo ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Wilayani Kilolo, Mlawa Cup imedhihirisha kuwa michezo inaweza kuleta si tu burudani, bali pia mafanikio ya muda mrefu kwa vijana na jamii kwa ujumla.
Ni muhimu kwa viongozi wa wilaya na wadau wa michezo kuendelea kuunga mkono mabonanza haya ili kuhakikisha kuwa michezo inabaki kuwa nguzo ya maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
KWA HABARI NA MAKALA MBALI MBALI ENDELEA KUFUATILIA MATUKIO DAIMA APP,MATUKIO DAIMA BLOG NA MATUKIO DAIMA TV (ONLINE) PIA MITANDAO YOTE YA KIJAMII NA USIKOSE KUSOMA GAZETI LA MWANAHABARI NA MACHINGA KILA SIKU IWAPO UNAHITAJI KUTANGAZA NASI PIGA SIMU 0754026299 EMAIL: matukiodaima3@gmail.com
0 Comments