Header Ads Widget

HONGERA SALIM ABRI ASAS KUTEULIWA KUWA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM TAIFA - JASMINE NG'UMBI


Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mufindi, Jasmine Ng’umbi, ametuma salamu za pongezi kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), ndugu Salim Abri Asas, kufuatia uteuzi wake kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.

 Jasmine amesema uteuzi huo ni heshima kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi, mkoa wa Iringa na kwa Watanzania kwa ujumla, huku akisisitiza kuwa Asas ni kiongozi anayestahili kwa dhati nafasi hiyo kutokana na mchango wake mkubwa ndani ya chama na jamii.


Jasmine ameeleza kuwa Salim Abri Asas amekuwa nguzo muhimu na kiongozi wa mfano ndani ya CCM mkoa wa Iringa, akijitolea kwa hali na mali kuhakikisha chama kinaimarika katika kila ngazi.

 Amesema uteuzi wake si wa bahati mbaya bali ni matokeo ya kazi nzuri, uaminifu na uadilifu wake ndani ya chama na jamii kwa ujumla. 

“Tuna kila sababu ya kujivunia uteuzi huu kwani umetufikisha mahali pa heshima kubwa kama mkoa wa Iringa,” amesema Jasmine.

Ameongeza kuwa kwa kipindi chote ambacho Asas amekuwa mstari wa mbele ndani ya chama, ameonyesha kuwa ni kiongozi mwenye maono, mvumilivu na mpenda maendeleo, ambaye muda wote amekuwa tayari kutoa mchango wake katika kuhakikisha chama kinaendelea kuwa na nguvu ya kisiasa na kijamii.

 Vilevile, amekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii kwa njia mbalimbali, ikiwemo kusaidia sekta ya elimu, afya, michezo na hata vijana ambao wamekuwa wakinufaika kupitia fursa mbalimbali alizowafungulia.

“Uteuzi huu unampa nafasi zaidi ya kuendeleza juhudi zake katika kuimarisha chama chetu kitaifa, lakini pia unatoa ujumbe kuwa CCM inatambua na kuthamini kazi nzuri zinazofanywa na viongozi wake kwa bidii na moyo wa kizalendo.

 Kwa kweli tunampongeza sana Mheshimiwa Asas na tunaamini ataendelea kulitumikia taifa kwa uadilifu, maarifa na moyo wa kizalendo kama alivyokuwa akifanya kabla ya uteuzi huu,” aliongeza Jasmine.

Aidha, Jasmine aliwataka vijana wa CCM kuiga mfano wa viongozi kama Salim Abri Asas, ambao wamekuwa wakitumia muda wao, vipaji na rasilimali katika kulitumikia taifa kupitia chama. 

Alisema kuwa mafanikio ya Asas yanapaswa kuwa chachu kwa vijana kujituma, kuwa na uadilifu, nidhamu na mapenzi ya kweli kwa chama na nchi yao.

 “Mafanikio haya hayakuja kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya kazi nzuri na kujitoa kwake kwa moyo mmoja. Tunapaswa kuyaona haya kama darasa kwetu vijana wa CCM,” alisema Jasmine.

Jasmine Ng’umbi alitoa wito kwa wanachama wote wa CCM kuendelea kumuunga mkono Salim Abri Asas katika majukumu yake mapya ndani ya Kamati Kuu ya CCM Taifa, kwani mafanikio yake ni mafanikio ya chama na jamii nzima ya Watanzania.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI