Na, Matukio daima App, Kilimanjaro.
MSIMAMIZI wa Uchaguzi katika halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Shadrack Mhagama amewataka wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea kushiriki kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ili kutimiza haki ya kikatiba ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Mhagama ametoa kauli hiyo leo wakati akitoa maelezo ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 kwa Watendaji wa Kata na Vijiji pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa katika ukumbi wa halmashauri ya Moshi.
Amesema kuwa, zoezi la kuandikisha wapiga kura litafanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 20 mwaka huu katika vituo vilivyopangwa na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi pindi muda utakapofika.
Msimamizi huyo wa Uchaguzi alisema kuwa, katika Uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu nafasi zitakazogombewa ni Mwenyekiti wa kijiji, Kitongoji, Wajumbe kundi mchanganyiko la Wanawake na Wanaume na wajumbe kundi la Wanawake.
Alisema kuwa, katika mamlaka ya Mji Mdogo wa Himo viongozi watakaochaguliwa ni Wenyeviti wa Vitongoji watakaounda Baraza la mamlaka ya Mji mdogo.
0 Comments