Header Ads Widget

MBUNGE NJEZA AENDELEA NA ZIARA MBEYA VIJIJINI, AHIMIZA ELIMU KWA WATOTO.

 

MBUMGE WA MBEYA VIJINI ORAN NJEZA KATIKA AMEWASHIKA MWANAFUNZI

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.


Wanafunzi wa Shule ya msingi Idimi kata ya Ihango wamepewa hamasa ya shilingi laki moja kwa kila mwanafunzi atakayepata ufaulu wa wastani wa 'A'.


Ahadi hiyo imetolewa na mheshimiwa Mbunge wa Mbeya vijijini Oran Njeza ambaye ametoa hamasa hiyo katika ziara yake anayoendelea nayo kijiji kwa kijiji katika kata na vijiji mbalimbali.



 MBUNGE ORAN NJEZA AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Idimi kata ya Ihango na baadhi ya wananchi waliofika shuleni hapo, Mbunge Njeza amewataka wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii huku Serikali ikiendelea kuboresha miundombinu ya utolewaji elimu ikiwemo kufikisha nishati ya umeme shuleni hapo.


Mbunge wa Mbeya vijijini amesema elimu ndiyo uwekezaji mzuri kwa watoto katika Dunia ya sasa na baadaye hivyo kuwaomba wananchi wenzake kuhakikisha wanasomesha watoto na kusisitiza suala la ulaji wa chakula cha mchana shuleni ili kuinua ufaulu.


"Asikwambie mtu bila elimu hakuna mtu atakayemsaidia mwenzake na ndio maana tunasema elimu ni ufunguo wa MAISHA, na mimi ninachowaambia mwalimu watakaofaulu kwa wastani wa A hata kama ni shule nzima hapa Idimi nitanunua kwa laki moja na msijeshangaa zawadi ikawa kubwa zaidi kwahiyo elimu ndio iwe baba na mama kwako", ameeleza Mbunge Oran Manasse Njeza wa Mbeya vijijini.



Diwani wa kata ya Ihango Mhe. Haustine Kwimba Mwandile, amemshukuru Mbunge kufanya ziara katani kwake na kumwomba kusaidia utatuaji wa kero ambazo bado zinazowakabili wananchi na wanafunzi hasa nishati ya umeme ambayo TANESCO wameahidi kushughulikia mapema iwezekanavyo kwani makosa yalitokea kutoanzia uwekaji nguzo kwenye taasisi hiyo ya umma wakati wa usambazaji nishati ya umeme.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI