Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limewaita vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani kujiunga na nafasi za mafunzo ya jeshi hilo kwa kujitolea huku likiwataadharisha wananchi kuepuka matapeli kwani mafasi hizo ni bure Haziuzi
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala (JKT) Kanali Juma Mrai amesema utaratibu wa Vijana kujiunga na hatimaye kuchaguliwa na mafunzo hayo unaratibiwa na ofisi za wakuu wa Mikoa na Wilaya ambapo mwombaji anaishi.
" Usaili wa Vijana kujiunga na mafunzo ya jeshi la kujeunga Taifa kwa kujitolea utaanza tarehe 01Oktoba 2024 kwa Mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani, " Amesema.
Na Kuongeza "Vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya jeshi la kujenga Taifa kuanzia tarehe 1 Novemba 2024 hadi Novemba 3 ,2024," Amesema Kanali Juma Mrai.
Aidha amesema Jeshi la kujenga Taifa linapenda kuwataarifu Vijana watakaopata fursa hiyo kuwa jeshi la kujenga Taifa kuwa halitoi ajira, pia halihusiki kuwatafutia ajira katika Asasi, vyombo vya ulinzi na Usalama na mashirika mbalimbali ya Serikali na ya sio ya kiserikali.
" Hivyo ifahamike kwamba Jeshi hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia Vijana kujiajiri wenyewe Mara baada ya kumaliza mkataba wao na jeshi la kujenga Taifa (JKT) , "Amesema Kanali Mrai.
Hata hivyo Kanali Mrai amesema Jeshi hilo halitahusika na utapeli wowote ambao utatokea na badala yake wafuate taratibu husika katika Ofisi ambazo zimeainishwa.
0 Comments